Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, amewaongoza familia na waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu) nyumbani kwake Tabata Segerea leo hii tarehe 15 Oktoba 2024.
Mwili wa marehemu, Meja Jenerali Charles Mbuge (mstaafu) unatarajiwa kuagwa kijeshi kesho tarehe 16 Oktoba 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na baada ya taratibu za kuagwa kijeshi kukamilika, Mwili huo utasafirishwa kuelekea mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika Oktoba 17, 2024