Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri mkuu asisitiza matumizi ya mifuko ya kielektroniki katika makusanyo

Waziri MkuuKassim Majaliwa amewataka maafisa masuhuli kwenye Halmashauri zote nchini waweke msisitizo wa kutumia mifumo ya kielektroniki katika makusanyo badala la kukusanya kwa fedha taslimu ‘Cash' Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza mapato katika maeneo yao na kuepuka vishawishi vya kutumia vibaya fedha za umma ambazo zinakusanywa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.  Amesema hayo leo (Jumamosi, Oktoba 05, 2024) alipozungumza kwenye kikao na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. “Suala la mapato ni lazima mliwekee msisitizo ili tupate matokeo mazuri kwenye halmashauri zetu. ” Mheshimiwa Majaliwa pia ametoa wito kwa wakurugenzi wa Halmashauri kutumia mapato ya ndani katika kutekeleza miradi ya maendeleo badala ya kusubiri fedha kutoka Serikali kuu pekee. “Acheni kutegemea mapato ya Serikali kuu pekee, tunataka kuona mapato ya ndani yanatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo. ” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka ...

Waziri Mkuu aanza ziara ya kikazi Temeke,Jijini Dar kwa kishindo

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 05, 2024 ameanza ziara ya kikazi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Mheshimiwa Majaliwa atakagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi wa umma.

WAZIRI MKUU KUANZA LEO ZIARA YA SIKU MBILI DAR

Katika ziara hiyo inayoanza asubuhi hii October 05 katika halmashauri ya wilaya ya Temeke,mh Waziri mkuu Kassim Majaliwa,atakutana na watumishi,kisha kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo kabla kufanya mkutano wa hadhara eneo la Mbagala rangi Tatu. Kesho ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake,mh Waziri mkuu atafanya ziara kama hiyo wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Gmtv George Marato akutana na mchezaji wa yanga Max Zengeli

Marato na Zengeli wamekutana baada ya kushiriki ibada ya maombi ya Pastor Tony,Millennium Tower's  jijini Dar es Salaam October 04-2024 

Serikali kulipa billioni 16 kuokoa shamba la ushirika mkoani pwani

  Na MWANDISHI WETU Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekubali yaishe baada ya kuridhia kulipa shilingi bilioni 16 ili kuliokoa shamba la ushirika wa wakulima wadogo wa umwagiliaji Ruvu Chauru, lililopo Mkoa wa Pwani.  Hayo yamebainika wakati Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe  akikagua maendeleo ya chama cha ushirika cha wakulima wa kilimo cha umwagiliaji Ruvu, Chauru Limited 2000, na kuzungumza na wakulima. “Shamba hili litapimwa kwa ushirikiano kati ya wizara na wilaya na mipaka yake itatambuliwa na kuwekwa alama za Tanroad”, amesema Waziri Bashe Bashe amesema kuwa Wizara ya Kilimo italipa fedha hizo zaidi ya shilingi bilioni 16 na kuweka makubaliano maalum na wakulima ili waendelee kutumia shamba hilo.  “Katika kata hii wakulima wanalima hekta 1800, sawa na zaidi ya hekari 2500,hivyo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC itatangaza tenda kwa ajili ya uwekaji wa miundombinu ya umwagiliaji na uzio ili wafugaji wasiingie ndani ya mashamba na wakulima walime kwa uhuru....

Wizara ya Madini,Tume ya madini na Bot yakutana na wadau wa madini

Ikiwa ni mkakati wa kujenga uelewa kwa wadau wa madini kuhusu utekelezaji wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini Sura 123, leo Oktoba 04, 2024 Wizara ya Madini imeratibu mkutano wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini uliofanyika jijini Dodoma ambapo elimu kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo imetolewa na wataalam kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Viongozi walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Kamishna Msaidizi – Uendelezaji Migodi, Mhandisi Ally Samaje aliyemwakilisha Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, Meneja wa Masoko ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Lameck Kakulu, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, CPA. Venance Kasiki na watendaji wengine kutoka Tume ya Madini. Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, Kamishna Msaidizi – Uendelezaji Migodi kutok...