Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dr Charles Mahera Awataka Makatibu wa Afya Mikoa na Halmashauri Kutatua Kero za Watumishi wa Afya

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Tamisemi Dkt. Charles Mahera amewaelekeza Makatibu wa Afya Mikoa na Halmashauri nchini kufuatilia, kushughulikia na kutatua kero za watumishi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe ili waweze kufanya kazi zao za kuwahudumia wananchi. Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afya ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Bi. Subisya Kabuje tarehe 23 Julai, 2024 mkoani Kigoma  wakati akiongea na timu ya usimamizi wa huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe katika ziara ya siku mbili inayoendelea mkoani humo. Amesema watumishi wa Afya ngazi ya vituo vya afya na zahanati wamekuwa na changamoto nyingi ambazo zinawakwamisha katika utekelezaji wa majukumu yao kila siku katika kuwahudumia wananchi hivyo zinapaswa kutatuliwa. Huku akitaja miongoni mwa changamoto hizo ni upandishwaji wa madaraja kwa watumishi wa Sekta ya Afya. Aidha amemtaka Afisa maendeleo ya jamii wa Manispaa ya Kigoma mjini kusimamia kwa ukaribu vikundi vya...

Shamrashamra za Miaka 60 ya JWTZ Zimeanza Baada ya Kuwasili Kwa Meli Vita Tatu Kutoka China

MELI vita tatu za kisasa kutoka Jeshi la Ukombozi la watu wa China,zimewasili katika Bandari ya Dar es Salaam zikiwa na askari na maafisa kadhaa wa jeshi hilo, kwa lengo la kushiriki na kufanya zoezi la pamoja la kivita na jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania JWTZ.  Akipokea meli hizo kwa niaba ya mkuu wa majeshi nchini, Mkuu wa kamandi ya jeshi la wanamaji Tanzania Rear Admiral Ameir Ramadhan, amesema Meli hizo za kijeshi zimekuja  nchini pamoja na mambo mengine zitashiriki kufanya zoezi la pamoja la kivita linajulikana Kwa jina la "AMANI UMOJA"  Kwa kuhusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  Zoezi Hilo la kivita linakwenda sambamba  na kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya ushirikiano Kati ya Tanzania China,ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ tarehe 01 Septemba 1964. Amesema zoezi hilo lita litashirikisha kamandi zote za JWTZ linatarajiwa kuanza 29 Julai 2024 na kumalizika tarehe 11 Agosti 2024. Amesema  w...

Waziri Kairuki Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani

Na Mwandishi Wetu - Zambia Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism) Kanda ya Afrika, Bi. Elcia Grandcourt. Pamoja na mambo mengine  kikao hicho kilijikita katika kuendeleza ushirikiano na Shirika hilo hususan, fursa na programu mbalimbali za  chombo hicho katika maeneo ya uendelezaji wa mazao ya utalii, utangazaji utalii, kuvutia uwekezaji katika miundombinu ya utalii na huduma, utoaji wa mafunzo na kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya utalii. Kikao hicho kilimefanyika leo  katika Hoteli ya Avani Victoria Falls Resort, Jijini Livingstone Zambia na  kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kitaalam wa UN, Bw. Jaime Mayaki,  Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii,  Bw. Richie Wandwi pamoja na Afisa Utalii wa UN Tourism, Bi. Zineb Remmal.

Majaliwa: Serikali ina Mahusiano Mazuri Na Sekta Binafsi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema maendeleo yaliyopo nchini hivi sasa yametokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya Serikali na sekta binafsi. “Maendeleo tunayoyaona nchini kwetu katika kila sekta yanategemea mchango wa Serikali pamoja na sekta binafsi. Dhamira na maono ya Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuimarisha sekta binafsi ili ihuishwe na kuwa mshindani katika kuleta maendeleo makubwa kwa nchi yetu,” amesema. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumanne, Julai 23, 2024) wakati akizungumza na wadau wa sekta binafsi nchini kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sekta Binafsi Tanzania kwa mwaka 2024 yaliyofanyika Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.  Wiki ya Sekta Binafsi Tanzania inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 25 ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). Amezitaka wizara na taasisi za Serikali ziendelee kupokea maoni ya sekta binafsi na kuhakikisha yanazingatiwa katika marekebisho ya sera na sheria za biashara ili kuondoa vikwazo vya urasimu na...

Mhandisi Rogatus Mativila Azitaka Halmashauri Zote Nchini Kusafisha Barabara na Mitaro

Serikali imezitaka Halmashauri zote nchini kutambua kuwa jukumu la kusafisha  barabara na mitaro ni la kwao na si la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) huku wananchi wakihimizwa kuzitunza barabara zinazojengwa katika maeneo yao. Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI  anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa barabara na madaraja zilizojengwa kwenye kata ya Kibakwe wilayani Mpwapwa. Mhandisi Matavila amesema kwamba Halmashauri zielewe kwamba suala la kusafisha barabara zilizojengwa kwenye Halmashauri, Miji na Majiji yao ni jambo la kwao na hivyo wanatakiwa kuhamasishana  waweze kusafisha. “Tumeshaletewa barabara nzuri tuzitunze ili zitusaidie sisi wenyewe, mwananchi una nyumba hapo pembeni ya barabara ni vyema kujitoa kusafisha hizo nyasi kandokando ya barabara”, amesisitiza

George Marato Tv Yapata Mwaliko Kushuhudia Mapokezi ya Meli Vita Tatu Toka China

Kituo cha Cha habari za Mtandaoni Cha George Marato TV  leo Julai 24,2024 kimekuwa ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyopata mwaliko wa mapokezi ya Meli vita tatu za Jeshi la Uukombozi wa watu wa  China. George Marato Mkurugenzi Mtendaji wa George Marato Tv ni Miongoni Mwa wawakilishi wa Vyombo Vya habari hapa Nchini vilivyopata mwaliko Kushuhudia Mapokezi hayo Katika bandari ya Dar es Salaam. Ujio wa meli vita hizi tatu ni kutoka Jeshi la ukombozi la watu wa China inatokana na ushirikiano ulipo na jeshi la ulinzi wa wananchi Tazania JWTZ ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jwtz