MELI vita tatu za kisasa kutoka Jeshi la Ukombozi la watu wa China,zimewasili katika Bandari ya Dar es Salaam zikiwa na askari na maafisa kadhaa wa jeshi hilo, kwa lengo la kushiriki na kufanya zoezi la pamoja la kivita na jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania JWTZ.
Akipokea meli hizo kwa niaba ya mkuu wa majeshi nchini, Mkuu wa kamandi ya jeshi la wanamaji Tanzania Rear Admiral Ameir Ramadhan, amesema Meli hizo za kijeshi zimekuja nchini pamoja na mambo mengine zitashiriki kufanya zoezi la pamoja la kivita linajulikana Kwa jina la "AMANI UMOJA" Kwa kuhusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
Zoezi Hilo la kivita linakwenda sambamba na kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya ushirikiano Kati ya Tanzania China,ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ tarehe 01 Septemba 1964.
Amesema zoezi hilo lita litashirikisha kamandi zote za JWTZ linatarajiwa kuanza 29 Julai 2024 na kumalizika tarehe 11 Agosti 2024.
![]() |
Amesema wakati JWTZ ikitimiza miaka 60 ya kuanzishwa kwake, Jeshi la ukombozi la Watu wa China linashiriki katika sherehe hizo ikiwa ni sehemu ya kudumisha undugu na mashirikiano.
Tukio hilo limehudhuriwa na balozi wa China nchini Bi Chen Mingjian, ambae amesema Tanzania na China ni nchi rafiki na zimekuwa na mahusiano ya muda mrefu.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Kamandi ya Jeshi la wana Maji nchini,amesema zoezi hilo ni mwendekezo wa ushirikiano ambapo kwa mara ya kwanza, zoezi kama hilo lilifanyikia Kigamboni na zoezi la pili lilifanyika mwaka 2019-2020 maeneo ya Mapinga na zoezi la tatu lilifanyika septemba mwaka jana.
Katika mapokezi hayo yalipambwa na vikundi mbalimbali vya burudani huku likishuhudiwa na baadhi ya maafisa na askari wa jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania.
![]() |










Comments
Post a Comment