Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewataka watumishi wa umma kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano kupitia michezo ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi kwa uadilifu.
Waziri Makonda ametoa kauli hiyo Septemba 26, 2026 wakati akifungua rasmi Michezo ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), inayofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro ikishirikisha jumla ya watumishi 2,771 kutoka wizara, mikoa, taasisi, idara na wakala wa Serikali.
Mashindano hayo yameanza Septemba 20 na yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 7, 2026, yakilenga pia kuwawezesha watumishi kushiriki katika shughuli za michezo na kuimarisha afya na mahusiano kazini.




Comments
Post a Comment