Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC),Itikadi,Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi amewataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kuilinda na kutunza amani na utulivu vilivyopo vispotee,kwani vikipotea kuvirejesha tena sio kazi rahisi.
Rai hiyo ameitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya lamore alipokuwa akihutubia wananchi na wanachama wa CCM ikiwa ni katika kuhitimisha ziara yake katika mkoa wa Tanga.
Aidha Kihongosi ameendelea kusema kuwa wanaochoea vurugu familia zako mara zote huwa salama na wanaoathirika ni wananchi wa hali ya chini hivyo basi ni jambo la kulitafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi yatakayo chochea uvunjifu wa amani.
"Niwaombe sana ndugu zangu wa Tanga kuendelea kuwa na utulivu huu mliouonesha kipindi chote kwani hata oktoba 29 mwaka jana Tanga ilikuwa salama,sehemu yoyote yenye amani na utulivu maendeleo huonekana nadio maana hata miradi ya kimkakati na maendeleo inakuka Tanga sasa kama ujenzi wa Bomba,mradi wa gesi na mingineyo,naendelea kuwasihi msidanganyike mkaivuruga amani hii",amesisitiza Kihongosi.
Kihongosi pia amewatahadharisha wanachama wa CCM kutojihisisha na rushwa kipindi Cha chaguzi za ndani zinazotarajiwa kufanyika mwakani na watakao bainika kufanya hivyo hatua Kali zitachukuliwa dhidi Yao.
Awali akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Serikali katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa umezidi kuifungua Tanga kiuchumi na kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Ameishukuru Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwekeza fedha nyingi ndani ya mkoa wa Tanga ikiwemo barabara zinazounganisha mkoa huo na Mikoa mingine ikiwemo barabara ya Tanga hadi Bagamoyo pamoja na ile ya kutoka Tanga mpaka Singida zote zikiwa zinaendelea kujengwa kwa kiwango la Lami.



Comments
Post a Comment