Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TPDC KUIJENGA TANGA KUWA KITOVU CHA BIASHARA YA MAFUTA


 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza kuweka mkazo katika kuendeleza Mkoa wa Tanga kuwa kitovu cha biashara ya mafuta nchini, kupitia mpango wa kujenga miundombinu ya kuchakata na kuhifadhi mafuta ghafi na safi pamoja na mabomba ya kusafirisha mafuta.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mussa Makame, amesema hayo leo, Septemba 21, 2026, jijini Dodoma, wakati akieleza mafanikio ya Shirika kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na miradi na mipango inayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/27.

Amesema mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa ushirikiano na kampuni za UNOC na Vitol Bahrain, unahusisha ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi (Refinery), maeneo ya kuhifadhia mafuta ghafi na safi, mabomba ya kusafirisha mafuta pamoja na miundombinu mingine wezeshi.

"Baada ya kusainiwa kwa Hati za Makubaliano (MoU) kati ya washirika wa mradi, tayari timu za kuratibu zimeundwa na zimeanza kazi za maandalizi zitakazowezesha utekelezaji wa mradi huo". Amesema



Akizungumzia maendeleo ya sekta ya mafuta nchini, Makame amesema TPDC inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati, ikiwemo Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ambao Tanzania inamiliki asilimia 15.

Amesema ujenzi wa EACOP umefikia asilimia 92.7, huku ukitarajiwa kuanza kupokea tone la kwanza la mafuta katika Pump Station Na. 1 nchini Uganda mwezi Desemba 2026.

"Baada ya hapo mafuta yataanza kusukumwa kupitia bomba hadi Chongoleani, Tanga, ambako yanatarajiwa kufika Februari 2027 kabla ya kuhifadhiwa katika matenki manne yenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya mapipa milioni mbili". Amesema

“Baada ya kukamilika kwa majaribio ya uwezo wa matenki kuhifadhi mafuta, upakiaji wa shehena ya kwanza ya mafuta ghafi kwenye meli unatarajiwa kuanza mwezi Machi 2027,” ameongeza.

Amesema utekelezaji wa EACOP umeendelea kutoa fursa kwa Watanzania kupitia ajira, biashara na kandarasi, ambapo jumla ya ajira 10,000 zimezalishwa katika kipindi cha ujenzi, kati yake 7,500 sawa na asilimia 75 zikiwa kwa Watanzania.

Aidha, amesema kampuni zaidi ya 200 za Kitanzania zimepata kandarasi za kusambaza bidhaa na huduma zenye thamani inayozidi Sh1.325 trilioni, huku Serikali ikiwa imekusanya zaidi ya Sh100 bilioni kupitia kodi, ada, ushuru na tozo mbalimbali.

Kwa upande wa uzalishaji wa gesi asilia, Makame amesema TPDC kwa kushirikiana na waendeshaji wa vitalu vya Songosongo na Mnazi Bay imeendelea kuzalisha wastani wa futi za ujazo milioni 170 kwa siku, sehemu kubwa ikitumika kuzalisha umeme na nyingine katika viwanda, taasisi na majumbani.

Amesema TPDC pia imefanikiwa kuchoronga visima vitatu katika Kitalu cha Mnazi Bay, ambapo viwili vya kuongeza uzalishaji tayari vimekamilika na kuunganishwa kwenye mfumo wa uzalishaji, vikiwa na uwezo wa kuzalisha kwa pamoja takribani futi za ujazo milioni 65 za gesi kwa siku.

Ameongeza kuwa kisima cha tatu cha utafiti kimekamilisha uchorongaji na kwa sasa taarifa zake zinaendelea kuchambuliwa ili kubaini uwepo na kiwango cha gesi.

Katika Kitalu cha Ruvuma, eneo la Ntorya, amesema TPDC inaendelea na uendelezaji wa gesi iliyogunduliwa pamoja na ujenzi wa bomba la gesi kutoka Ntorya hadi Madimba, Mtwara.

"Bomba hilo lenye kipenyo cha inchi 14 na urefu wa kilomita 34.2 litakuwa na uwezo wa kusafirisha hadi futi za ujazo milioni 140 za gesi kwa siku. Mradi huo wenye thamani ya Sh122.7 bilioni umefikia asilimia 67 na unatarajiwa kukamilika katika robo ya mwisho ya mwaka 2026". Amesema

Makame amesema TPDC pia inaendelea na utafutaji wa mafuta na gesi katika Kitalu cha Lindi-Mtwara kupitia uchukuaji wa taarifa za mitetemo kwa mfumo wa 3D katika eneo la takribani kilomita za mraba 736. Mradi huo wenye thamani ya Sh107 bilioni umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kukamilika Julai 2027.

"Katika Kitalu cha Eyasi-Wembere, TPDC imekamilisha uchukuaji wa kilomita 779 za taarifa za mitetemo kwa mfumo wa 2D na inaendelea na awamu ya pili yenye urefu wa kilomita 325.7, huku mradi mzima ukitarajiwa kugharimu Sh53 bilioni". Amesema

Kwa upande wa gesi asilia, amesema TPDC imeendelea kupanua matumizi yake kwa kuunganisha nyumba 1,000 katika mikoa ya Pwani na Lindi pamoja na viwanda viwili katika mwaka wa fedha 2025/26.

Amesema Shirika pia linaendelea na mpango wa kufikisha gesi katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na Arusha kupitia mabomba, CNG na teknolojia ya Mini-LNG.

Kuhusu Mini-LNG, amesema TPDC iko katika mazungumzo na kampuni sita za wawekezaji, ambapo tayari imesaini makubaliano ya mauziano ya gesi asilia na kampuni tatu zinazotarajiwa kutekeleza miradi hiyo katika maeneo yasiyofikiwa na miundombinu ya mabomba.

Akizungumzia mafanikio ya kibiashara, Makame amesema TPDC ilipata faida ya Sh72.98 bilioni katika mwaka wa fedha 2025/26, huku ikilipa kodi ya Sh50.04 bilioni, mgawo wa faida na mrabaha wa Sh142.61 bilioni na gawio la Sh15.118 bilioni kwa Serikali.

Amesema Shirika pia lilishiriki na kushinda zabuni sita za uagizaji wa mafuta kupitia mfumo wa pamoja unaoratibiwa na PBPA na, katika kipindi cha Mei hadi Julai 2026, lilipewa jukumu la kuingiza mafuta yote nchini, ambapo jumla ya meli 34 ziliwasili kwa ratiba iliyopangwa.

Kwa upande wa miradi ya kijamii, amesema TPDC inaendelea na ujenzi wa kivuko cha kisasa katika Kisiwa cha Songosongo chenye thamani ya takribani Sh5.7 bilioni, ambacho ujenzi wake umefikia asilimia 55 na kinatarajiwa kukamilika Novemba 2026.

Aidha, amesema Shirika linaendelea na ujenzi wa vituo vya afya vya Dihimba na Madimba mkoani Mtwara vyenye thamani ya takribani Sh2.4 bilioni, pamoja na miradi ya maji, elimu na afya katika maeneo mbalimbali.

Makame amesema ongezeko la mahitaji ya gesi asilia nchini limevuka uwezo wa sasa wa uzalishaji katika vitalu vya Songosongo na Mnazi Bay, jambo ambalo TPDC inalichukulia pia kama fursa ya kuongeza uzalishaji na kuendeleza maeneo mapya ya gesi.

Amesema katika mwaka wa fedha 2026/27, TPDC itaweka mkazo katika kuongeza uzalishaji wa gesi katika Songosongo na Mnazi Bay, kuendeleza gesi ya Ntorya, kukamilisha bomba la Ntorya–Madimba na kuendelea na utafutaji katika vitalu vya Lindi-Mtwara, Eyasi-Wembere, Songosongo Magharibi na Mnazi Bay Kaskazini.

“Mwelekeo wa Shirika ni kuhakikisha tunaweka nguvu, jitihada na rasilimali zetu katika kuongeza uzalishaji wa gesi asilia na upatikanaji wake ili kukidhi mahitaji makubwa ya gesi hapa nchini na nchi za jirani,” amesema.

Amesema TPDC itaendelea pia kuongeza wateja wa gesi katika viwanda, taasisi na majumbani, huku ikisisitiza matumizi ya teknolojia za mabomba, CNG na Mini-LNG ili kufikisha nishati hiyo katika maeneo mengi zaidi nchini.

Ikumbukwe kuwa Miradi hiyo inaendelea kufungua fursa za ajira, ujuzi, zabuni na uwekezaji kwa Watanzania, hususan vijana, katika maeneo ya uhandisi, ujenzi, usafirishaji, ugavi, teknolojia na huduma za kitaalamu.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...