Imeelezwa kuwa namna ya kufikisha na kufanikisha *Utekelezaji wa Dira 2050* ni kuwepo na uundaji wa Kamati za Usimamizi, Ufuatiliaji na Utekelezaji kwenye ngazi zote pamoja na mkakati mawasiliano utumiwe ipasavyo kufikisha ujumbe kwa viongozi na wananchi.
Hayo yameelezwa na *Mhe. Jumanne Abdallah Sagini* Agosti 20, 2026 wakati alipokuwa akitoa *Mafunzo ya Kujenga Uwezo wa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Songwe kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050* katika Jukwaa la Dira yenye mada ya "Uongozi wa Kimkakati na Mabadiliko ya Fikra Kiuongozi na Kiutendaji katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuwezesha Utekelezaji wa Dira 2050"
*Sagini* ameeleza kuwa kufanikisha kwa *Dira 2050* hakutegemei fedha tu bali watu wakiwemo viongozi, Watendaji katika Sekta binafsi ambapo viongozi watendaji watasaidia kutafsiri Dira katika mipango mikakati inayotekelezeka.
"Mabadiliko ya fikra kwetu sote ni injini ya kutufikisha kwenye matokeo tarajiwa na ajenda ya utekelezaji wa *Dira 2050* iwe ya kudumu katika vikao vyote muhimu ambapo Utekelezaji wa DIRA utaendelea hata viongozi wakibadilika na wananchi kujiandaa kwa fursa mbalimbali kwani Dira hii ina fursa nyingi kwa kuijua na mikakati ya utelezaji wake wananchi watajiandaa kushiriki na kutumia fursa ziłizopo kukua kiuchumi," ameeleza *Mhe. Sagini*.
Aidha amempongeza *Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Omari Makame* kwa juhudi za awali za utekelezaji wa *Dira 2050* ambapo ameeleza kuwa uelewa wa aina moja huwafanya wote kujua mwelekeo na kutekeleza mipango, miradi na kazi zitakazofikisha kwenye matokeo tarajiwa ili Kuepusha viongozi na watendaji kupingana kwa kuwa wote wanafahamu viongozi kwa viongozi na watendaji kwa watendaji hawatavutana katika maamuzi na utendaji wa kazi.







Comments
Post a Comment