Kikao hicho kimefanyika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa ambapo pamoja na mambo mengine amewapongeza machifu hao kwa juhudi zao za kuhifadhi eneo hilo muhimu kwa Taifa katika utunzaji wa mazingira.
Hifadhi ya Misitu ya Miteremko ya Safu za Milima ya Lyamba Lyamfipa ina vyanzo vingi vya maji ambayo yanatumiwa na wananchi kwa matumizi ya nyumbani na kwenye kilimo cha umwagiliaji na pia ndio chanzo cha mvua kwa eneo la Sumbawanga.