Kutoka: Dawati la Habari Polisi Mwanza. Askofu wa Kanisa la TGC, Robert Bundala amewataka wananchi kuiona Jeshi la Polisi kama sehemu ya jamii na si chombo kilicho mbali nao huku akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa dini, Polisi na wananchi ni muhimu katika kuimarisha amani na usalama. Askofu Bundala ameyasema hayo Oktoba 08,2026 wakati wa ziara ya watumishi wa dini waliotembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na kukabidhi mipira kwa ajili ya shughuli za michezo, hatua iliyolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Polisi na jamii. Amesema viongozi wa dini na Jeshi la Polisi wana majukumu yanayokaribiana katika kuelimisha jamii, kuzuia maovu na kuwasaidia watu kurejea katika mwenendo mwema. Amesema viongozi wa dini wanashirikiana na Polisi katika masuala mbalimbali, ikiwemo kutoa elimu kwa jamii na kushiriki katika kukemea uovu, shughuli za ulinzi na usalama, hususan katika maeneo ya nyumba za ibada. “Polisi si watu waliotoka Mbinguni. Polisi ni ndugu...
Marato tv - Sauti ya Jamii