Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

IPU 153: ZUNGU AKUTANA NA 12 PLUS GROUP ARUSHA

 Rais wa Mkutano wa 153 wa IPU na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), amekutana na wajumbe wa umoja wa kundi la Kijografia na Kisiasa (12 Plus Group). Mazungumzo yao yamelenga  kuratibu sera, mitazamo, na msimamo mbalimbali inayojadiliwa kwenye mkutano wa 153  wa IPU. Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 8 Oktoba, 2026 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC).

IGUWASA YAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL-NINO IGUNGA

Na Mwandishi Wetu – Tabora MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga Mjini (IGUWASA), imeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El-Nino zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya mabomba ya maji katika maeneo hatarishi. Hatua hiyo inahusisha kuweka kingo za udongo katika maeneo yanayopitiwa na mabomba ya maji, pamoja na kuandaa vifaa vya dharura vitakavyotumika endapo kutatokea uharibifu wa miundombinu kutokana na mvua hizo. Mkurugenzi Mtendaji wa IGUWASA, Alexander Ntonge, amesema maandalizi hayo yanalenga kuhakikisha huduma ya maji inaendelea kupatikana kwa wananchi hata wakati wa mvua hizo. Ntonge pia amewataka wananchi kuchukua tahadhari, ikiwemo kuhifadhi maji ya kutosha kabla na wakati wa mvua hizo, pamoja na kutumia maji safi na salama ili kuepuka magonjwa ya mlipuko. Amesema wananchi wanapaswa kutoa taarifa haraka wanapoona uharibifu wa miundombinu ya maji, ili hatua za kurekebisha ziweze...

RAIS SAMIA APELEKA TABASAMU KWA WASANII TOZO ZIKIPUNGUZWA

Na Mwandishi Wetu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza marekebisho ya kanuni ambazo zimepunguza utitiri wa tozo na kupunguza kwa kiwango kikubwa kiwango cha ada walizokuwa wakitozwa wasanii na wanaofanya shughuli za sanaa kwa mwaka. Hayo yalitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Edward Buganga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu marekebisho hayo ya kanuni. Alisema marekebisho ya tozo hizo kwa mwaka 2026 yalifanywa na Bunge zinazolenga kuimarisha usimamizi wa Sanaa, kuwawezesha wasanii na wadau wa Sanaa, na kupunguza utitiri wa tozo. Alisema kanuni hizi ambazo tayari zimeanza kutumika na tunawakumbusha wadaua kuwa hazilengi kuzuia ubunifu na zinaweka utaratibu unaolinda wasanii, hadhira, watoto, urithi wa Sanaa na maslahi ya wadau, huku ikiwezesha sekta kukua na kushindana ndani na nje ya nchi.  Alisema mabadiliko hayo ya kanuni yanahusu wasanii na vikundi vya Sanaa, maDJs, washereheshaji, maproduza, Mameneja,...

MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI AWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA COP12 YA MKATABA WA NAIROBI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12), leo tarehe 08 Oktoba 2026. Mkataba wa Nairobi (Nairobi Convention) unalenga kuimarisha uhifadhi, usimamizi endelevu na ulinzi wa mazingira ya bahari na ukanda wa pwani katika eneo la Magharibi mwa Bahari ya Hindi. Mkutano huo, ulioanza tarehe 06 Oktoba 2026 na unaotarajiwa kuhitimishwa tarehe 09 Oktoba 2026, unafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya Mkataba wa Nairobi, ulioanzishwa mwaka 1985. Aidha, mkutano huo unalenga kujadili mikakati ya kukuza uchumi wa buluu kupitia uvuvi endelevu, kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ya bahari na athari za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuimarisha uhifadhi wa bayoanuai za baharini na maeneo ya pwani.

DKT. MWIGULU AZUNGUMZA NA WAWAKILISHI WA SPACEX NA STARLINK

 Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amezungumza na wawakilishi wa Kampuni za SpaceX na Starlink kuhusu uwekezaji wa kampuni hizo nchini Tanzania katika sekta ya mawasiliano na teknolojia. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt, London, Uingereza, Oktoba 7, 2026, na kuhudhuriwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Angela Kairuki; Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Musa Omar; pamoja na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo.

PBZ YANUFAIKA NA MABORESHO YA BANDARI TANGA.

  Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Maboresho ya Bandari ya Tanga yaliyoghalimu zaidi ya Shilingi Bilioni 429.1 Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) imekuwa ni miongoni mwa wanufaika wakuu kupitia tawi lake lililopo mkoani hapa ambapo wananchi wanaotumia usafiri wa majini na shughuli za uvuvi wamekuwa wadau wao wakubwa. Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Benki ya watu wa Zanzibar tawi la Tanga Wahbi Ali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa wafanyabishara waliopo kati ya Tanga na Zanzibar pamoja na wavuvi wanaotumia Majahazi wamekuwa wakiitumia benki hiyo kukopa kwaajili ya biashara zao. Aidha Wahbi ameongeza kuwa muitikio kwa wanatanga ni mzuri tangu walipofungua tawi katika mkoa huu na hii imetokana na mahusiano ya karibu yaliyopo kati ya Tanga na Zanzibar. "Tangu tumefungua huduma yetu katika mkoa wa Tanga muitikio umekuwa ni mzuri  ukilinganisha na mahusiano ya ukaribu yaliyopo kati ya Tanga na Zanzibar muingiliano wa kibishara uliopo imetusaidia kuanza vizuri na...