SERIKALI imefungua fursa ya Sh5 bilioni kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wabunifu wenye kampuni changa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ikilenga kugeuza mawazo na bunifu zao kuwa biashara zinazokua, ajira na masoko mapya. Fursa hiyo imetolewa kupitia Programu ya Uwezeshaji wa Mikopo kwa Kampuni Changa za TEHAMA iliyozinduliwa jijini Dodoma, ambapo Serikali imesema fedha hizo zitatolewa kwa kampuni zitakazokidhi vigezo na masharti yaliyowekwa. Akizindua programu hiyo, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema Serikali inalenga kuona mikopo hiyo ikileta matokeo yanayoonekana katika ukuaji wa kampuni, ongezeko la ajira, mauzo na mapato pamoja na upanuzi wa masoko ndani na nje ya Tanzania. “Swali letu si tu tumetoa mikopo kiasi gani? Swali muhimu zaidi ni fedha hizo zimeleta mabadiliko gani?” amesema. Amesema mikopo hiyo itatolewa katika madaraja matatu, kuanzia Sh1 milioni hadi Sh25 milioni, zaidi ya Sh25 milioni hadi Sh50 milioni na zaidi ...
Marato tv - Sauti ya Jamii