Mkurugenzi wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Fredrick Salukele amesema ushiriki Tanzania katika mashindano ya ujuzi ya WorldSkills umefungua fursa mpya za kimataifa kwa vijana wenye ujuzi, huku tayari washiriki wawili wakikubaliwa kwenda Shanghai, China kama waangalizi wa Mashindano ya WorldSkills International 2026. Akizungumza wakati wa Mashindano hayo yanayoendelea jijini Tanga, Selukele amesema vijana hao wanatoka katika fani za mtandao wa vitu na urembo tiba, hatua inayoonesha kuwa ujuzi wa Tanzania umeanza kutambulika kimataifa. "Baada ya matokeo ya mashindano ya kitaifa kutangazwa, Tanzania itawasilisha washindi kwa WorldSkills ili kuitangazia dunia kuwa nchi yetu ina taasisi zinazozalisha wahitimu wenye ujuzi unaokidhi viwango vya kimataifa,"amesema. Amesema kuonekana katika majukwaa ya WorldSkills kunawaongezea vijana nafasi za ajira za kimataifa, huku Serikali ikilenga kuanzisha mfumo wa vyeti vinavyotambulik...
Marato tv - Sauti ya Jamii