MBUNGE wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara ameibana Serikali kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa ajili ya barabara zinatumika kwa kazi hiyo pekee huku akitaka wakandarasi wanaojenga chini ya kiwango kuwajibishwa kwa kuisababishia Serikali hasara kubwa. Waitara amesema hayo leo Mei 21, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, ambapo alieleza kuwa wananchi wa Tarime, Serengeti na Mkoa wa Mara kwa ujumla wanaendelea kupata adha kubwa kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara. Amesema barabara ya kilomita 87 kuelekea Mgumu Serengeti ambayo tayari imeanza kujengwa bado inakabiliwa na changamoto kubwa baada ya baadhi ya wakandarasi kuondoka eneo la mradi kutokana na ukosefu wa fedha, hali inayosababisha watalii na wananchi kupata usumbufu mkubwa wanaposafiri katika maeneo hayo muhimu ya kiuchumi na utalii. Mbunge huyo pia ametaja barabara muhimu zinazohitaji maboresho haraka kuwa ni pamoja na Musoma–Makoko, Musoma–Bunda, Tarime–Serengeti, Mtegi–Sirari pamoja n...
Marato tv - Sauti ya Jamii