Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Yonazi Atoa Wito Kwa Wananchi Kutumia Vituo Vya Maarifa Kujua Hali Zao za Afya

Na Mwandishi Wetu -Morogoro Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, ametoa wito kwa wananchi kutumia Vituo vya Maarifa ili kupata huduma mbalimbali za afya na kufahamu hali zao za kiafya, hususan kuhusu maambukizi ya VVU na UKIMWI. Dkt. Yonazi ametoa wito huo leo Mei 19, 2026, wakati wa ziara ya kukagua utendaji wa Vituo vya Maarifa vya Dumila mkoani Morogoro na Kibaigwa mkoani Dodoma. Akizungumza baada ya kutembelea vituo hivyo, Dkt. Yonazi alisema Serikali itaendelea kuimarisha na kusambaza Vituo vya Maarifa katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata huduma za ushauri nasaha, elimu ya afya na upimaji bila malipo. “Nitoe wito kwa wananchi wetu kuendelea kutumia Vituo vya Maarifa kwa wingi ili waweze kupata ushauri, huduma na elimu mbalimbali ya afya, hususan kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Serikali itaendelea kuweka vituo hivi kote nchini,” alisema Dkt. Yonazi. Aidha, alisema Serikali ina mpango...

Wabunge Watoa Pongezi Kwa Rais Samia Kwa Kuimarisha Amani na Utulivu Nchini

Wabunge mbalimbali wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha amani, usalama na heshima ya nchi ndani na nje ya mipaka yake. Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma, Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Selemani Jafo amesema Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha amani kutokana na uongozi imara wa Rais Samia pamoja na uwekezaji mkubwa katika sekta ya ulinzi na usalama. Jafo amesema uimara wa vyombo vya ulinzi na usalama umeiwezesha Tanzania kuheshimika kimataifa, huku Jeshi la Wananchi wa Tanzania likiendelea kuwa nguzo muhimu katika kulinda amani ndani na nje ya bara la Afrika. “Rais Samia ameonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa salama, tulivu na kuheshimika kimataifa kupitia uimarishaji wa sekta ya ulinzi na usalama,” amesema Jafo. Katika mchango wake, a...

Katundu

Na. Sgt. Geofrey Jacka - DODOMA Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, CP. Nicodemus Tenga, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, CGP. Jeremiah Yoram Katungu, Mei 19, 2026 amefungua Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Mali za Kudumu za Serikali (GAMIS), akieleza kuwa kufanyika kwa mafunzo hayo ni utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. CP. Tenga amesema, katika kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi kwa Maafisa Magereza, Mei 9, 2026 Ukonga Dar Es Salaam, Rais Dkt. Samia, aliekeleza Jeshi la Magereza kutumia TEHAMA katika utendaji wake ili kuongeza ufanisi na uwazi serikalini na kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia. Aidha, CP. Tenga, amesema ni matarajio ya Jeshi  baada ya mafunzo hayo, wataalamu wa ununuzi watakuwa na maarifa mapya ya kutumia mfumo wa GAMIS na kuwaongezea uelewa wa Sheria na Kanuni za usimamizi wa mali za kudumu za Serikali, kuongeza uwajibikaji, kuboresha utunzaji wa kumbukumbu na kuimarisha u...

CGP Katundu-Mafunzo ya Mfumo wa

Serikali Kuendelea Kuboresha Vituo vya Maarifa Nchini

Na, Mwandishi wetu - Pwani SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuboresha Vituo vya Maarifa nchini, hususan vile vinavyotoa huduma kwa madereva wa malori ya masafa marefu kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi mapema mwanzoni mwa wiki mara baada ya kutembelea na kukagua Vituo vya Maarifa vinavyotoa huduma za VVU na UKIMWI kwa madereva wa malori ya masafa marefu vilivyopo eneo la Kurasini  katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam na Mdaula mkoa wa Pwani ambayo Vituo hivyo vipo chini ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS). Dkt. Yonazi amesema Serikali, kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), ina jukumu la kusogeza huduma muhimu za VVU na UKIMWI karibu na wananchi. “Vituo hivi vina mchango mkubwa katika kuwafikia madereva wa masafa marefu ambao mara nyingi hukaa safarini kwa muda mrefu. Serikali itaendelea kuviboresha hususan...

Mwili wa Baharia Mtanzania Aliyefariki Uae Wawasili Nchini

Mwili wa Baharia Mtanzania, Bw. Mchama Maregesi Mongu, aliyefariki dunia akiwa kazini nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), umewasili nchini Mei 18, 2026 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Mwili huo ulipokelewa na viongozi wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu waliokuwepo uwanjani hapo. Baharia Mongu alifariki dunia Mei 3, 2026 baada meli ya kuvuta ya VOLANS (tug boat) aliyokuwa akifanya kazi kushambuliwa kwa bomu katika Mlango wa Bahari wa Hormuz ilipokuwa safarini kutoka UAE kuelekea Oman.  Akizungumza baada ya kupokea mwili huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nahodha Mussa Mandia, ameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Konseli Kuu ya Tanzania - Dubai kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kufanikisha taratibu zilizowezesha kuurejeshwa ngumbani nwa mwili wa marehemu Mongu. Nahodha Mandia pia ametoa rai kwa wamiliki wa vyombo vya...