Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mavunde Atoa Wito Kwa Benki Nchini Kutengeneza Mikopo Maalum Kwa Wachimbaji Wadogo

● Mhe. Rais  Samia apongezwa kwa kuweka mazingira wezeshi ya biashara, ● Serikali yaweka mkakati wa kuwawezesha mitaji wachimbaji wazawa ● Upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji wadogo kuwezesha ukuaji wa uchumi  Geita, Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* atoa wito kwa benki zote nchini kuchangamkia fursa kwenye sekta ya madini kwa kubuni na kutengeneza bidhaa maalum ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kuwa na mitaji itakayoongeza tija kwenye shughuli zao. Ameyasema hayo leo tarehe 09 Mei, 2026  alipokuwa akizindua Tawi la Benki ya Exim Mkoani Geita. "Ninamshukuru kwa dhati *Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa namna anavyoendelea kuisimamia sekta ya madini. Maono na maelekezo yake ndiyo yanaifanya sekta ya madini kukua kwa kasi na kupelekea mchango wake kwenye Pato la Taifa kufikia asilimia 10.1" "Nitoe wito kwa benki zote nchini, kufikiria kuwa na bidhaa maalum kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo pasipo kuathiri masharti ya Sheria ya Fedha. Niwaomb...

Dkt. Mwigulu Afungua Soko la Mazao Kibakwe, Dodoma

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumamosi (Mei 9, 2026) ameweka jiwe la msingi la ufunguzi wa soko la mazao Kibakwe, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma. Ujenzi wa soko hilo umelenga kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kupata maeneo rasmi, salama na yenye miundombinu stahiki kwa ajili ya biashara ya mazao yao. Akizungumza na wananchi baada ya uzinduzi wa soko hilo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amejitambulisha kuwa kiongozi wa matokeo kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa moja kwa moja maisha ya Watanzania “Mheshimiwa Dkt. Samia ni  mtendaji. Ambaye akisema jambo, anatekeleza. Na haya yanadhihirishwa kwa kazi kubwa ambayo imefanyika” Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amefanya kazi kubwa inayowapa heshima Watanzania wote. “Nchi inapopiga hatua, kwa kazi kubwa inayofanywa Rais wetu, inalinda heshima ya uhuru wa nchi”.

Tanzania na Canada kuimarisha uhusiano kwenye utafiti wa Madini

■ Waziri Mavunde aeleza fursa zilizopo kwenye utafiti, ■ Balozi Burns abainisha utayari wa Makampuni ya Canada kuwekeza nchini Tanzania, ▪️Canada yaonesha utayari wa kusaidia teknolojia kwa wachimbaji wadogo  ■ *Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais yaweka Mazingira wezeshi kwa wawekezaji  nchini. *Dodoma* Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania, *Mheshimiwa Emily Burns* katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo katika jengo la Tume ya Madini, Kilimani Jijini Dodoma. Katika mazungumzo hayo, Waziri Mavunde alibainisha kuwa moja ya kipaumbele kikuu cha sekta ya madini ni utafiti ambao utapelekea kutambua aina na kiwango cha rasilimali madini tulizobarikiwa nchini kwetu na kuvutia uwekezaji. "Tunafamu kuwa Nchi yetu tumeweza kufanya utafiti wa kina wa kurusha ndege kwa asilimia 16 tu. Hivyo, tuna uhitaji mkubwa wa kupata uwekezaji zaidi katika eneo hili ili kuongeza mchango wa sekta ya madini kweny...

Baraza la Wafanyakazi ni nguzo ya Ushirikishwaji wa Watu,Mhe.Millya

Imeelezwa   kuwa   Mikutano   ya   Mabaraza   ya   Wafanyakazi   ni majukwaa   muhimu   ya   kuwashirikisha   watumishi   moja   kwa   moja katika mipango ya Serikali ili kupata mawazo mapya na umiliki wa pamoja wa mipango hiyo kwa lengo la kutekelezwa kwa ufanisi na bila manung’uniko.  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika   Mashariki  (EAC),   Mhe.  James   Millya   wakati  anafungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma Mei 08, 2026. Mhe. Millya alisema kitendo cha Baraza hilo kupitia makadirio ya bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 kitawapa watumishi fursa ya kupitia maeneo muhimu ya vipaumbele vilivyowekwa na kuboresha mikakati   ya   utekelezaji  ...

Dkt. Mwigulu Aagiza Itafutwe Suluhu ya Kudumu Daraja la Magole–Dumila

  _▪️Ateta na WanaGairo, asisitiza kuitunza amani_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya ukaguzi wa daraja la Magole lililopo Dumila katika Mto Mkundi wilayani Kilosa na kuagiza uongozi wa TANROADS utafute suluhu ya kudumu ya changamoto inayolikabili daraja hilo ya kujaa maji na mchanga kila mwaka. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Mei 8, 2026) wakati akizungumza na wananchi waliofika darajani hapo kumsikiliza na akamtaka Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro ashirikiane na wataalamu wengine kuandaa utaratibu wa kuwaruhusu wananchi kuchimba mchanga katika eneo hilo kwa kuzingatia maelekezo ya kitaalamu, ili kusaidia kupunguza mzigo wa gharama za Serikali na wakati huohuo kulinda miundombinu ya daraja hilo. “Meneja wa TANROADS na wenzako wote ratibuni eneo ambalo tunahangaika kutoa mchanga na hatuna bajeti, wananchi muwaruhusu watoe mchanga huo kwa utaratibu wa kitaalamu,” amesisitiza Waziri Mkuu. Akitoa taarifa kuhusu hali ya eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Mal...

Wizara ya Viwanda na Biashara Yaahidi Kuendelea Kukuza Ubunifu na Ujasiriamali Kwa Vijana

Na MATUKIO DAIMA APP MOROGORO  Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imeahidi kuendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha vijana nchini kukuza vipaji vyao vya ubunifu pamoja na shughuli za ujasiriamali, hatua inayolenga kuongeza ajira, kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Aristides Mbwasi, amesema hayo wakati alipomwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Judith Kapinga, katika hafla ya kufunga maadhimisho ya Siku ya Mzumbe sambamba na Kambi ya Ujasiriamali iliyofanyika katika Chuo Kikuu Mzumbe.  Mbwasi amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na vijana katika kukuza uchumi kupitia bunifu mbalimbali wanazoziibua kila siku, hivyo itaendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi za elimu ya juu pamoja na wadau wengine wa maendeleo ili kuhakikisha ubunifu huo unakuwa na tija kwa jamii na taifa. Amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho dunia imejaa ushinda...