Baraza la Wafanyakazi ni nguzo ya Ushirikishwaji wa Watu,Mhe.Millya

GEORGE MARATO TV
0


Imeelezwa   kuwa   Mikutano   ya   Mabaraza   ya   Wafanyakazi   ni majukwaa   muhimu   ya   kuwashirikisha   watumishi   moja   kwa   moja katika mipango ya Serikali ili kupata mawazo mapya na umiliki wa pamoja wa mipango hiyo kwa lengo la kutekelezwa kwa ufanisi na bila manung’uniko. 

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika   Mashariki  (EAC),   Mhe.  James   Millya   wakati  anafungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma Mei 08, 2026.


Mhe. Millya alisema kitendo cha Baraza hilo kupitia makadirio ya bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 kitawapa watumishi fursa ya kupitia maeneo muhimu ya vipaumbele vilivyowekwa na kuboresha mikakati   ya   utekelezaji   wake  kwa   kuzingatia   Sera,   Mikakati   na Mipango iliyopo.

Mhe.   Millya   alitaja   mafanikio   mbalimbali   kupitia   utekelezaji   wa mpango   wa   utekelezaji   wa   Mwaka   wa   Fedha   2025/2026   ambao utakamilika Juni,  30   2026.  Mafanikio hayo ni  pamoja   na  teuzi za nafasi  za kikanda  na  kimataifa ikiwa  ni  pamoja uteuzi  wa  Katibu Mkuu   wa   Jumuiya   ya   Afrika   Mashariki,   Balozi   Stephen   Mbundi; kuimarika kwa  taswira   na  heshima ya Tanzania   katika   nyanja ya kimataifa; kuimarika kwa ushirikiano wa uwili, kikanda na kimataifa; na kuongezeka kwa mchango wa Watanzania waishio nje ya nchi.

Mafanikio mengine ni  kuanza  kwa ujenzi  wa  Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mlima Kilimanjaro; ujenzi na ukarabati wa ofisi na makazi ya Balozi nje ya nchi; na kulinda usalama wa Watanzania nje ya nchi na kuwarejesha salama kutoka kwenye maeneo yenye changamoto za usalama.

Naibu   Waziri   Mallya   alisisitiza   umuhimu   wa   Wizara kuzingatia vipaumbele vya Serikali kuelekea utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ambayo utekelezaji wake utaanza mwaka wa fedha ujao.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top