● Mhe. Rais Samia apongezwa kwa kuweka mazingira wezeshi ya biashara, ● Serikali yaweka mkakati wa kuwawezesha mitaji wachimbaji wazawa ● Upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji wadogo kuwezesha ukuaji wa uchumi Geita, Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* atoa wito kwa benki zote nchini kuchangamkia fursa kwenye sekta ya madini kwa kubuni na kutengeneza bidhaa maalum ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kuwa na mitaji itakayoongeza tija kwenye shughuli zao. Ameyasema hayo leo tarehe 09 Mei, 2026 alipokuwa akizindua Tawi la Benki ya Exim Mkoani Geita. "Ninamshukuru kwa dhati *Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa namna anavyoendelea kuisimamia sekta ya madini. Maono na maelekezo yake ndiyo yanaifanya sekta ya madini kukua kwa kasi na kupelekea mchango wake kwenye Pato la Taifa kufikia asilimia 10.1" "Nitoe wito kwa benki zote nchini, kufikiria kuwa na bidhaa maalum kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo pasipo kuathiri masharti ya Sheria ya Fedha. Niwaomb...
Marato tv - Sauti ya Jamii