Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wanu Hafidh awasilisha Randama ya Bajeti ya Wizara ya Elimu 2026/27

Baada ya trilioni 2.44 za mwaka wa fedha 2025/2026, wizara ya Elimu kufungua pazia la bajeti mpya kesho Mei 07, 2026 Leo Mei 06, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidhi Ameir amewasilisha Bungeni jijini Dodoma  randama za makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/ 2027 ikiwa ni hatua ya awali kuelekea hotuba rasmi hapo kesho Mei 07, 2026 Ikumbukwe kwamba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika bajeti iliyopita iliomba na kuidhinishiwa Sh trilioni 2.44 kwa mwaka 2025/2026, sasa macho yote yako kwenye bajeti ya 2026/2027 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni kesho.

REA Yawezesha Vikosi vya JKT Kukuza Matumizi ya Nishati Safi

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu ametoa wito kwa vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vilivyopata miradi ya nishati safi ya kupikia kuwa mabalozi wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii zinazowazunguka. Mwenyekiti Kingu ametoa wito huo leo Mei 5, 2026 wakati wa ziara ya Bodi hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia inaayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Kambi ya JKT ya Maramba mkoani Tanga. Aidha, amesisitiza vijana wanaliopo kwenye kambi hizo za JKT kupatiwa mafunzo ya namna ya kutengeneza mkaa mbadala ili waweze kutumia ujuzi huo kujiajiri na kuwa mawakala wa kutengeneza mkaa mbadala pindi watakapomaliza mafunzo yao. Kwa upande wake, akimwakilisha Mkuu wa JKT, Kanali Projest Rutaihwa aliishukuru menejimenti na Bodi ya REA kwa utekelezaji wa miradi nishati safi ya kupikia huku akiahidi kusimamia mradi huo unakuwa endelevu ili kuendelea kulinda mazingi...

Geita Regional Commissioner to Officiate Tanzania’s World Donkey Day 2026

By Prosper Makene Geita Regional Commissioner, Mr Martin Shigela will officiate this year’s national World Donkey Day celebrations on Friday, May 8, 2026, at Mgusu Ward in Geita Municipal Council.  The United Republic of Tanzania, through the Ministry of Livestock and Fisheries, is hosting the event to highlight the vital role donkeys play in rural livelihoods. The announcement was made yesterday by the Ministry in Dodoma through an official public notice, emphasizing the government’s commitment to animal welfare and rural development. Caring for Donkeys is Our Collective Responsibility This year’s theme underscores the economic and social value of donkeys across Tanzania and Africa. The theme was adopted following the African Union Heads of State Summit held in Dar es Salaam in October 2022. During that summit, 32 African nations officially recognized donkeys as critical to the continent’s transport, agriculture, and household economies, and pledged to strengthen protections again...

Mkuu wa Mkoa wa Geita Kufungua Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Punda Duniani 2026

Na Prosper Makene Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigela, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Punda Duniani yatakayofanyika Ijumaa, Mei 8, 2026, katika Kijiji Cha Mgusu, Kata ya Mgusu, Halmashauri ya Manispaa ya Geita. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, inaandaa tukio hilo kuangazia mchango mkubwa wa punda katika maisha ya vijijini. Tangazo hilo lilitolewa jana na Wizara jijini Dodoma kupitia taarifa rasmi kwa umma, likisisitiza dhamira ya Serikali katika ustawi wa wanyama na maendeleo ya vijijini. *Kumtunza Punda ni Jukumu la Sote*   Kaulimbiu ya mwaka huu inasisitiza thamani ya kiuchumi na kijamii ya punda nchini Tanzania na Afrika nzima. Kaulimbiu hiyo ilipitishwa kufuatia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika Dar es Salaam mwezi Oktoba 2022. Katika mkutano huo, mataifa 32 ya Afrika yalitambua rasmi kuwa punda ni nguzo muhimu ya usafirishaji, kilimo, na uchumi wa kaya barani Afrika, na ...

MMI Yaimarishwa Misungwi: Wakuu wa Idara Wakumbushwa Umuhimu wa Kujibu Hoja za CAG

 Na Thomas Lutego ; Misungwi  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi.Peniel Titus ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mipango wa Halmashauri hiyo amefungua Mafunzo ya MMI na Amesisitiza Umuhimu wa Mafunzo Hayo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo kwani ndio Sehemu za kujibu Hoja za CAG ambapo Mafunzo hayo ni Muhimu kwa Halmashauri Katika kutekeleza Shughuli mbalimbali za Miradi. Mkufunzi wa MMI Mkoa  wa Mwanza Bw. Kusire Swai ameeleza kuwa Mafunzo hayo ni Marefu hivyo yanahitaji Umakini Na Ufuatiliaji. Hivyo ni Vyema Kufuata Sheria,Kanuni,Taratibu na Miongozo na ni Muhimu Mafunzo haya Wapewe wakuu wa Idara na Vitengo  kwani Mafunzo haya ya hoja ni Muhimu  kwani chanzo cha hoja ni kuanzisha Mradi na ndio wahusika wa hoja. Amesisitiza kwa Sasa Hoja zote zitajibiwa kwenye Mfumo ambao Umeboreshwa na TAMISEMI.

Samia Aendeleza Diplomasia ya Michezo, Akutana na Didier Drogba Dodoma

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo akiwa Ikulu jijini Dodoma amekutana na nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea F.C. na Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba, pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda. Mkutano huo unaangaliwa kama sehemu ya kuimarisha diplomasia ya michezo (sports diplomacy), ambapo ushirikiano kati ya serikali na mastaa wa kimataifa unatumika kukuza sekta ya michezo kama kichocheo cha ajira, uwekezaji na utalii wa michezo nchini.