Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Akagua Maendeleo ya Ujenzi wa Uwanja Mpira wa Miguu, Arusha.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 17, 2026 amekagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo mkoani Arusha ambao utatumika kwa ajili ya michuano ya AFCON 2027 itakayofanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Bushiri Yaifunga Masaika, Aweso Vijana Cup

NA - MWANDISHI WETU, PANGANI  Mashindano ya Aweso Vijana Cup yameendelea kwa kasi ambapo Aprili 16, 2026, yalizikutanisha timu kutoka Kata ya Bushiri na Masaika ambapo Bushiri ilipata ushindi wa (1-0), mechi iliyochezwa katika uwanja wa Shule ya Sekondari Masaika. Katika mechi hiyo, Timu ya Bushiri ilipata goli lake la ushindi kupitia kwa mchezaji wake, Rashid Taube, dakika ya 15 ya mchezo. Mratibu wa mashindano hayo, Ramadhani Kibendera amesema mashindano hayo yameongezeka hamasa ya vijana kupenda michezo. "Mwamko ni mkubwa, vijana wa Pangani wanajitokeza sana katika mashindano haya, na yamesaidia sana kupunguza idadi ya vijana kujiingizia katika makundi mabaya, sasa michezo imekuwa sehemu muhimu ya maisha yao," amesema Kibendera. Mashindano ya Aweso Vijana Cup yanahusisha timu kutoka Kata zote 14 za wilaya ya Pangani, chini ya udhamini wa Mbunge wa Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Pembejeo Nafuu na Teknolojia Kuinua Tasnia ya Pamba – Chongolo

WAZIRI wa Kilimo,Mheshimiwa Daniel Chongolo, amesema Serikali imeboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo ili kuhakikisha zinawafikia wakulima kwa wakati na kwa gharama nafuu, hatua inayolenga kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo. Akizungumza leo Aprili 16, 2026 jijini Dodoma katika mkutano wa wadau wa tasnia ya pamba uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre. “Serikali imeboresha mifumo ya pembejeo ili kuhakikisha wakulima wanapata kwa wakati na kwa bei nafuu, jambo litakalosaidia kuongeza uzalishaji na tija.” Ameongeza kuwa Sera ya Kilimo ya mwaka 2023 inaelekeza kila kijiji kuwa na Afisa Ugani mmoja ili kuwasaidia wakulima kitaalamu ambapo mkutano huo unaongozwa na kauli Mbiu isemayo “Nguvu ya Pamoja kwa Tasnia ya Pamba Endelevu,”. “Dhamira yetu ni kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Afisa Ugani, hatua itakayosaidia wakulima kupata elimu sahihi na kuongeza uzalishaji hadi kufikia malengo ya mwaka 2030,” alisema Chongolo. Aidha, amewahimiza wakulima...

Serikali na Wadau wa Pamba Tanzania, Wajifungia Katika Kuweka Mkakati wa Kuongeza Uzalishaji wa Zao Hilo