WAZIRI wa Kilimo,Mheshimiwa Daniel Chongolo, amesema Serikali imeboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo ili kuhakikisha zinawafikia wakulima kwa wakati na kwa gharama nafuu, hatua inayolenga kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo.
Akizungumza leo Aprili 16, 2026 jijini Dodoma katika mkutano wa wadau wa tasnia ya pamba uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre.
“Serikali imeboresha mifumo ya pembejeo ili kuhakikisha wakulima wanapata kwa wakati na kwa bei nafuu, jambo litakalosaidia kuongeza uzalishaji na tija.”
Ameongeza kuwa Sera ya Kilimo ya mwaka 2023 inaelekeza kila kijiji kuwa na Afisa Ugani mmoja ili kuwasaidia wakulima kitaalamu ambapo mkutano huo unaongozwa na kauli Mbiu isemayo “Nguvu ya Pamoja kwa Tasnia ya Pamba Endelevu,”.
“Dhamira yetu ni kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Afisa Ugani, hatua itakayosaidia wakulima kupata elimu sahihi na kuongeza uzalishaji hadi kufikia malengo ya mwaka 2030,” alisema Chongolo.
Aidha, amewahimiza wakulima kuendana na teknolojia za kisasa katika shughuli za kilimo.
“Ni wakati wa wakulima wetu kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza ubora na ushindani wa mazao yetu sokoni,” amesisitiza
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania, Marco Mtunga, ameeleza umuhimu wa kuboresha mfumo wa ushirika:
“Mfumo wa ushirika unahitaji maboresho ya kina ili uweze kuwasaidia wakulima kwa ufanisi zaidi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Christopher Gachuma amesisitiza umuhimu wa tija katika uzalishaji amabpoa amesema Siri kubwa ya mafanikio ipo kwenye tija.
"Ni muhimu viongozi wa mikoa kutoa elimu kwa wakulima ili wazalishe kwa ufanisi,”. Amesema Gachuma.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emanuel Cherehani, ameshauri Serikali kuimarisha usimamizi wa vyama vya ushirika.
“Ni muhimu kuwa na mfumo madhubuti wa kusimamia vyama vya ushirika ili kuongeza tija na mapato kwa wakulima wa pamba,” amesema Cherehani.
Mkutano huo uliobeba kaulimbiu “Nguvu ya Pamoja kwa Tasnia ya Pamba Endelevu,” ulilenga kuimarisha ushirikiano wa wadau katika kukuza sekta ya pamba nchini.

.jpg)
.jpg)













.jpg)



