Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu: Mheshimiwa Lukuvi Alikuwa Mshauri Kwa Watu Wengi

_Asema alikuwa na kiwango cha juu cha kujitolea_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema enzi ya uhai wake, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Isimani, Mheshimiwa William Lukuvi alikuwa mshauri kwa watu wengi wakiwemo wabunge na mawaziri. “Mimi ni mmojawapo wa watu walionufaika na ushauri wake tangu nikiwa Naibu Waziri wa Fedha na hata sasa alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu aliendelea kunishauri kwa karibu zaidi,” amesema. “Alikuwa na kiwango cha juu cha kujitolea, atakumbukwa sana kama mshauri na mlezi wa kila mmoja, na kwa muda mrefu nimekuwa mmojawapo kati ya wengi walionufaika na busara zake.” Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 27, 2026) wakati akizungumza katika ibada ya kumuombea marehemu na kisha kuwaongoza viongozi wa Serikali, Wabunge na waombolezaji kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Amesema tabia ya kujitolea kwa muda mwingi bila kuchoka ilimp...

Walimu 150 wa Amali Kwenda India Jumapili kwa Mafunzo Maalum

Na Mwandishi Wetu WALIMU 150 wa amali kwenye shule za serikali wanaondoka Jumapili kwenda nchini India kwa mafunzo maalum ya amali ambayo yatawawezesha kuongeza ujuzi kwenye taaluma hiyo. Walimu hao kutoka mikoa mbalimbali nchini waliagwa rasmi jana kwenye hafla maalum iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali. Waliagwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe na Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link, (GEL) Abdulmalik Mollel. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga walimu hao, Profesa Mkenda alisema safari hiyo ni maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza kuboreshwa kwa elimu ya amali. Profesa Mkenda alisema kwa kuwa wameanza kutoa mafunzo hayo ya amali ikiwemo kwenda kujifunza kwenye mataifa mbalimbali duniani hakutakuwa na kurudi nyuma. “Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza mara kadhaa kuhusu mafunzo ya amali, anataka kuona t...

Wanaotaka Urais Kabla ya Muda Kunaweza Kuigawa CCM-Wassira

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewaonya wanachama walioanza harakati za kusaka urais mwaka 2030 kwa kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujawadia, hivyo wanaofanya hivyo wanakiuka kanuni, miongozo na utaratibu. Amesema kuanza mapema harakati za kusaka uongozi kabla ya wakati inaweza kukigawa Chama badala ya kukijenga hivyo inapaswa kukemewa. Wasira ameeleza hayo leo Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi za CCM Wilaya ya Bunda ambazo zilichomwa moto katika na vurugu za Oktoba 29, 2025. Alisema ndani ya Chama kuna kundi la wanachama ambao hawana kazi za msingi ndani ya CCM zaidi ya kujihusisha na makundi ya kisiasa. Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti Wasira, kundi hilo limeanza kujipanga kwa kuunda safu kuanzia ngazi za kata, hali ambayo inaweza kusababisha mgawanyiko ndani ya CCM kwa kuwa kila mmoja anataka kuwa na wafuasi wake badala ya kuimarisha umoja. Wasira alihoji uhalali wa baadhi ya watu kuan...

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Jkt Awasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara Yake

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho (Mb), Tarehe 26 Machi 2026,  Bungeni jijini Dodoma amewasilisha kwa kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mambo ya nje, ulinzi na Usalama-NUU , taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi Cha kuanzia julai 2026 hadi Februari 2027. Kamati hiyo ya NUU inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Nasma Murtaza Giga (Mb) pia ilipokea taarifa ya Wizara ya Ulinzi na JKT na mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Ulinzi ya SUMMA JKT, MZINGA na NYUMBU. Waziri wa Ulinzi na JKT katika uwasilishaji wa taarifa hiyo ya utekelezaji wa bajeti kwa kamati ya NUU aliambatana na viongozi waandamizi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo , Dkt.Faraji Kasidi Mnyepe

Mradi wa Dmdp II Kujenga Kilomita 42.78 za Lami Kigamboni

Dar es Salaam  Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara Kilomita 42.78 kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika kata za Mjimwema, Kibada, Kigamboni, Vijibweni na Somangila zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni. Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Kigamboni, Mhandisi Edgar Tumsifu ambapo amesema kuwa mradi huo unaogharimu shilingi Bilioni 110 utekelezaji wake umefikia asilimia 30 huku tayari umeshaanza kuleta matokeo kwani barabara zilizokuwa na changamoto zimeshaanza kufanyiwa kazi na zikikamilika wananchi watanufaika na miundombinu hiyo. "Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi huu, TARURA Kigamboni tuna mtandao wa barabara Km 1035 kati ya hizo barabara za lami ni Km 10 lakini kupitia DMDP II imetuletea Km 42.78 kwahiyo tutakuwa na zaidi ya Km 50 za barabara za lami mpaka kufikia ...

HESLB yatilia mkazo PPP kutanua wigo wa ufadhili wa wanafunzi

Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga Elimu ni gharama. Elimu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji fedha ili kuyakamilisha ili kupata utulivu wa kujifunza darasani. Serikali inasimamia na kutekeleza kikamilifu Sera ya Elimumsingi Bila Ada ambapo hutumia fedha nyingi kuwezesha upatikanaji wa mahitaji muhimu shuleni ili shughuli za ufundishaji na ujifunzaji ziweze kufanyika vizuri na kuwapunguzia mzigo wazazi na walezi gharama za kusomesha watoto wao. Kupitia Sera ya Elimumsingi Bila Ada, fedha zinawafikia walengwa ipasavyo. Serikali hutuma fedha moja kwa moja katika akaunti za benki za shule ili zigharimie masuala mbalimbali ya kuendesha shule kama vile shughuli za utawala, taaluma, mitihani, ukarabati, michezo na mahitaji mengine kadha wa kadha. Sambamba na hilo, serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatoa ufadhili kwa wanafunzi wanaosoma Stashahada kwa kozi za kipaumbele, Shahada ya kwanza na kuendelea katika kozi mbalimbali ili kwa pamoja vijana wa Kitanzan...