Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Yaimarisha Upatikanaji wa Mafuta ya Petroli Nchini Malawi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Serikali kupitia Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuwa nguzo muhimu ya upatikanaji wa mafuta kwa nchi jirani ya Malawi, hatua inayochochea shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi hizo mbili. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miundombinu ya mafuta katika Kituo cha Kurasini Oil Jet (KOJ-1), kilichopo katika Bandari ya Dar es Salaam, Waziri wa Nishati na Madini wa Malawi, Mhe. Dkt. Jean Mathanga, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika kuwezesha mtiririko wa mafuta kwenda nchini Malawi. Alisema kuwa kutokana na Malawi kutokuwa na bandari, nchi hiyo inategemea kwa kiasi kikubwa miundombinu ya nchi jirani, hususan Tanzania, katika kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unaendelea kuwa wa uhakika. Alibainisha kuwa ziara hiyo imelenga kujionea kwa vitendo namna mafuta yanavyopokelewa na kusimamiwa bandarini ili kuboresha mipango ya ununuzi na usambazaji wa mafuta nchini Malawi.  Kwa upande wake, Mwakilishi wa...

Kongole NECTA kwa mpango kupanda miti 150,000 kutunza mazingira

Na: Dk. Reubeni Lumbagala Utunzaji wa Mazingira ni jukumu letu sote. Uwe mtoto, kijana, mtu mzima au mzee. Uwe mwanamke au mwanamme, uwe msomi au usiwe msomi, suala la utunzaji mazingira linakuhusu. Faida za utunzaji mazingira zinatunufaisha sote. Madhara ya uharibifu mazingira yanatuathiri sote. Hakuna aliye salama mazingira yakiharibika. Ndiyo maana ni vyema mikakati ya utunzaji mazingira ikafanyika mapema. Dunia kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Kutokana na changamoto hiyo, mikakati inawekwa ya namna bora ya kukabiliana na changamoto hiyo ili kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi na kufurahia maisha. Tanzania kwa kuwa si kisiwa, tumeathirika pia na mabadiliko ya tabianchi kama zilivyo nchi nyingine. Serikali imechukua hatua kadhaa ikiwemo suala la kuhamasisha watu binafsi, taasisi, makampuni na wizara kupanda miti ili kupunguza athari. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa mfano mzuri wa kuigwa kuanzia kuhamasisha watu kupanda miti hadi kufanya kwa ...

Mgodi wa Kihistoria wa Niobium kujengwa mkoani Mbeya

▪️Ni Mradi wa Panda Hill wa Niobium utakaogharimu TSh 700 bn ▪️Ni uwekezaji unaohusisha Kampuni ya Denham ya Marekani. ▪️Rais Samia apongezwa kufanikisha mradi wa uchimbaji Niobium ▪️Kiwanda cha kuyeyusha ferroniobium kitakachojengwa Tanzania kitakuwa cha nne duniani ▪️Waziri Mavunde asema Tanzania kuchangia takriban asilimia 4 ya uzalishaji wa Niobium na uzalishaji wa takriban tani 100,000 kwa mwaka ▪️Ajira  kufikia takriban  watu 7,000 MBEYA, Machi 24, 2026 — Tanzania imeingia hatua muhimu ya kuimarisha biashara na Marekani baada ya Serikali na Panda Hill Tanzania Limited kusaini mkataba wa makubaliano ya kuendeleza Mradi wa Niobium wa Panda Hill, hatua inayolenga kuifanya Mbeya kuwa kitovu cha uzalishaji na usindikaji wa madini mkakati. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde alisema mradi huo ni wa uzalishaji wa madini adimu ambayo hayapatikani kila mahali duniani, na kwamba Tanzania inalenga kuchukua nafasi ya kipekee katika soko la kima...

Waziri Makonda Ashiriki Katika Kongamano la Kiswahili Duniani

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), linapofanyika Kongamano la Tano la Idhaa za Kiswahili Duniani, leo Machi 24, 2026.  Kongamano hilo limeandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), likiwakutanisha wadau wa lugha ya Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi, na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Serikali Yahimiza Meli ya New Mv Mwanza Kukuza Uchumi, Utalii Kanda ya Ziwa

‎Serikali imetoa wito kwa wafanyabiashara, wasafirishaji na wawekezaji mbalimbali kutumia fursa ya meli mpya ya MV New Mwanza kibiashara na kiutalii ili kukuza uchumi wa Kanda ya Ziwa. Itakumbukwa meli hiyo imejengwa kwa zaidi ya Tsh. Bilioni 120, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari makubwa matatu na madogo, ambapo itafanya safari zake katika bandari zote zinazozunguka Ziwa Victoria ikiwemo Kisumu (Kenya), Port Bay (Uganda) na Kemondo (Bukoba). ‎Akizungumza Jumapili Machi 22, 2026 na waandishi wa habari katika bandari ya Mwanza Kusini jijini Mwanza ilipoegeshwa meli hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Utamaduni ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kutokana na uwekezaji huo wakazi wa Kanda ya Ziwa, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanapaswa kuitumia kwenye shughuli zao na kuleta tija ya uwekezaji huo mkubwa. ‎ ‎Amesema Serikali imetimiza jukumu lake la kutekeleza wajibu wa kujenga mazingi...