Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tamasha la Pasaka Mwaka Huu Kupambwa na Wasanii Kutoka Nchi Mbalimbali

 Wasanii nguli wa nyimbo za Injili kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuungana na waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa nchini kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka ambalo huandaliwa na kuratibiwa na Kampuni ya Msama Promotions ambapo kwa msimu huu linatarajiwa kufanyika kwa mikoa 20 likianzia na Mkoa wa Dar es Salaam. Mapema akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama amesema msimu huu wa pasaka Tamasha hilo litaanza tarehe 5 ya mwezi wa nne,likizunguka katika mikoa 20,kutoa burudani likiwa limesheheni wasanii mbalimbali wakubwa kutoka Tanzania na nje ya Tanzania lengo ikiwa ni kuwapa burudani waumini wa dini ya kikristo na wasio wa kristo sambamba na kutoa ujumbe wa kiroho. Kadhalika Msama amesema wasanii wakubwa wanatarajiwa kupanda katika majukwaa hayo kutoa burudani kabambe kwa mikoa 20 kwani hiyo ni dhamira ya wao kama waandaji kuwapa burudani waumini wa Injili. Ikumbukwe Tamasha hilo ambalo huandaliwa na Msama Promotions limekuwa maarufu kwa...

Rais Atangaza Kuwateua Dkt Mpango na Majaliwa

  Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kumteua Makamu wa Rais mstaafu, Dkt Philip Mpango kuwa mshauri wake wa masuala ya uchumi na miradi. Pamoja naye, ametangaza kumemteua Waziri Mkuu mstaafu, Kassim Majaliwa kuwa mshauri wake wa masuala ya jamii. Hata hivyo, uteuzi wa wawili hao ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Dkt Samia wakati wa kampeni za uchaguzi, aliposema ataendelea kuwatumia wawili hao kwa shughuli za Serikali. Dkt Samia ametangaza uteuzi huo, leo Jumamosi Januari 10, 2026 wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa Ikulu ya Dar es Salaam. Amesema katikati ya Dkt Mpango na Majaliwa watakaomshauri kwenye masuala ya uchumi, miradi na jamii, kutakuwa na Profesa Palamagamba Kabudi akisema ndiye atakayefanya kazi nao kwa karibu. “Vile vichwa viwili vikubwa (Dk Mpango na Majaliwa) vinahitaji mtu aliyetulia anayeweza kudili nao.  Hawa watoto wangu mara wanaweza kujijibia ikaja kesi, lakini Profesa (Kabudi) anaweza kwenda nao vi...

Wananchi Zanzibar Waomba Masoko ya Madini

📍 Zanzibar | Januari 10, 2026 Wananchi wa Zanzibar wameiomba Serikali kupitia Tume ya Madini kuanzisha masoko na minada rasmi ya madini Visiwani humo ili kuwawezesha wafanyabiashara, wachimbaji wadogo na wawekezaji kufanya biashara ya madini kwa uwazi, usalama na bei shindani. Ombi hilo limetolewa na wananchi waliotembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar yanayoendelea kufanyika Fumba, ambapo wameeleza kuwa ukosefu wa masoko rasmi na minada ya madini umekuwa kikwazo kwao kushiriki kikamilifu katika biashara ya madini. Wamesema kuwepo kwa masoko na minada ya madini kutachochea ukuaji wa uchumi wa Zanzibar, kuongeza ajira kwa vijana na wanawake, kuongeza kipato kwa wananchi pamoja na kudhibiti biashara holela ya madini. Kupitia maonesho hayo, Tume ya Madini inaonesha fursa katika utafutaji wa madini, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani, biashara ya madini pamoja na utoaji wa bidhaa na huduma kwa shughuli za migodini. Akizungumza katika...

Waziri Kijaji Azindua Bodi ya Wakurugenzi ya Tawa*

Na Joyce Ndunguru, Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), ameizindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) leo Januari 9, 2026, jijini Arusha. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Dkt. Kijaji amewapongeza wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA kwa kuteuliwa kwao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko. “Kwa namna ya kipekee nikupongeza sana Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko kwa kuendelea kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa awamu nyingine tena. Kwa dhati ya moyo wangu, ninawapongeza wote kwa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi ya TAWA, hongereni sana”, amesema Waziri Kijaji. Sambamba na pongezi hizo, Waziri Kijaji ametoa rai kwa Bodi ya TAWA kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika uboreshaji wa miundombinu kwenye maeneo ya hifadhi, kwa lengo la kuyaongezea thamani,...

Rais Samia Azindua Hotel ya Kitalii Kusini Unguja Zanzibar

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Jaz Elite Aurora, Bw. Hamed El Chiaty kuashiria uzinduzi wa Hoteli hiyo katika hafla iliyofanyika Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Januari, 2026.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Hoteli ya Jaz Elite Aurora katika hafla iliyofanyika Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Januari, 2026.  Taswira ya Hoteli ya Jaz Elite Aurora iliyopo Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 09 Januari, 2026. 

Silinde: Awataka Wakandarasi Wazawa Wahakikishe Kunakuwa na Tija Katika Miradi ya Umwagiliaji

📍 Bariadi- Simiyu  Serikali imewataka wakandarasi wazawa wanaotekeleza miradi ya Umwagiliaji nchini kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa wakulima na taifa kwa ujumla, ikisisitiza kuwa uzembe au kuchelewesha utekelezaji kutaibua hatua kali za kisheria dhidi yao. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) akiwa katika muendelezo wa ziara yake mkoani Simiyu, wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji la Kasoli lililopo Kijiji cha Kasoli, Kata ya Kasoli. Bwawa hilo lina ujazo wa takribani mita za ujazo milioni 2.7 na linatarajiwa kuhudumia mashamba yenye ukubwa wa hekta 650. Mhe. Silinde amesema kuwa uamuzi wa Serikali kuwapa wakandarasi wazawa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo ya Umwagiliaji, unalenga kuwajengea uwezo na kukuza ujuzi wa ndani ili wazawa washiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao. Amesisitiza kuwa imani hiyo lazima iendane na uwajibikaji, ubora wa kazi na kukamilisha miradi kwa wakati uliopangwa. “Serika...