Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Dkt. Nchemba Aagiza Soko la Majengo Likamilike Kwa Wakati

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kukamilika haraka kwa ukarabati wa soko la Majengo Jijini Dodoma ili kuwawezesha wafanyabiashara wa jiji hilo kunufaika na mradi huo. Dkt. Nchemba ametoa maagizo hayo leo Alhamisi, Desemba 11, 2025 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kujionea maendeleo ya ukarabati wa soko hilo unaotarajiwa kukamilika Machi, 2026. Sambamba na hayo, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Fredrerik Sagamiko kuhakikisha kwamba wanatoa kipaumbele cha kugawa vizimba kwa wafanyabiashara waliokuwepo awali katika soko hilo.

Huduma za mkoba zaokoa watanzania wilaya za pembezoni

Na Mwanndishi Wetu Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marko, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wa pembezoni kupitia Kampeni ya Huduma za Mkoba za uchunguzi wa saratani zinazoendeshwa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI). Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tatu katika Hospitali ya Wilaya ya Serengeti,  Angelina alisema huduma hizo zimetoa fursa kubwa kwa wananchi kutambua afya zao kwa wakati. “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia kwa kutuwezesha kupata huduma hizi muhimu hapa Serengeti. Serikali inaendelea kuokoa maisha kwa kuhakikisha wananchi wa vijijini hawakosi huduma za kibingwa,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya. Aidha, alisisitiza kuwa Serikali ya Wilaya itahakikisha wananchi wote waliopata rufaa wanafika Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. “Hakuna mgonjwa wa Serengeti atakayekosa kufika Ocean Road kwa sababu ya kutokuwa na nauli. Tutahakikisha tunaokoa maisha ya wananchi wetu,” alisis...

Dkt. Mwigulu Ahani Msiba wa Marehemu Jenista Mhagama

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 11, 2025 amehani msiba wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama, Itega jijini Dodoma.

Mali na Madeni ya Viongozi wa Umma Kupitiwa Upya-Dkt Mwigulu

_Ataka maeneo yaliyokithiri kwa rushwa yapewe kipaumbele_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema ni lazima yafanyike mapitio ya haraka kwenye tamko la mali na madeni na yawe na madaraja kwa sababu kuna maeneo ambayo bado rushwa imekithiri lakini watumishi wake hawajajumuishwa kwenye mfumo kama viongozi wa umma. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Desemba 11, 2025), alipozungumza na Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, alipotembelea ofisi hizo zilizopo Mtaa wa Tambuka Reli, Jijini Dodoma. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhakikisha uadilifu unasimamiwa kuanzia katika sheria, kanuni na utekelezaji ili rasilimali za Taifa ziweze kuwanufaisha wananchi wote. Amesema kuwa yapo maeneo ambayo fedha za umma huwa zinapotea hivyo yawekewe uangalizi wa kutosha. “Bado kuna kazi kubwa katika usimamizi wa maadili ya umma, suala hili Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amelisisitizia sana” Amei...

Dkt. Mwigulu Azungumza na Viongozi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 11, 2025 amezungumza na watendaji na viongozi wa Sektretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo jijini Dodoma. Akizungumza na watendaji hao, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa yapo maeneo ambayo bado rushwa imekidhiri lakini watumishi wake hawatambuliki kama sehemu ya viongozi kwa majukumu yao. “Ni muhimu kufanya mapitio ya haraka ya tamko ili nao waweze kujumuishwa”

Uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu ya Jimbo la Butiama Katika Kata ya Kamuegegi

Tumezindua rasmi mchakato wa kuunda Timu ya Mpira wa Miguu ya Jimbo la Butiama, hatua ya kwanza ikiwa imefanyika leo katika Kata ya Kamugegi! Tukiwa na dhamira ya kuijenga Butiama kupitia michezo, umoja na kukuza vipaji vya vijana.  Uzinduzi huu umehudhuriwa na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Kamugegi, Wilson Kinguye, na Diwani wa kata ya Buruma mh Mogela Mbonosi pamoja na viongozi wengine wa Kata—ikiwa ni ishara ya mshikamano na malengo ya pamoja kwa maendeleo ya vijana wetu. Mchakato huu unaanzia katika ngazi ya Vijiji, kisha Kata—zikijumuisha Kata zote 18—hadi kupatikana kwa timu moja mahiri itakayolibeba na kuliwakilisha Jimbo la Butiama kwa heshima, nidhamu na ushindani. Huu ni mwanzo wa safari endelevu ya kuimarisha, uainishaji, ukuaji wa vipaji, ushirikiano, mshikamano kwa vijana, amani, umoja na afya njema kupitia nguvu ya michezo.