Tumezindua rasmi mchakato wa kuunda Timu ya Mpira wa Miguu ya Jimbo la Butiama, hatua ya kwanza ikiwa imefanyika leo katika Kata ya Kamugegi!
Tukiwa na dhamira ya kuijenga Butiama kupitia michezo, umoja na kukuza vipaji vya vijana.
Uzinduzi huu umehudhuriwa na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Kamugegi, Wilson Kinguye, na Diwani wa kata ya Buruma mh Mogela Mbonosi pamoja na viongozi wengine wa Kata—ikiwa ni ishara ya mshikamano na malengo ya pamoja kwa maendeleo ya vijana wetu.
Mchakato huu unaanzia katika ngazi ya Vijiji, kisha Kata—zikijumuisha Kata zote 18—hadi kupatikana kwa timu moja mahiri itakayolibeba na kuliwakilisha Jimbo la Butiama kwa heshima, nidhamu na ushindani.
Huu ni mwanzo wa safari endelevu ya kuimarisha, uainishaji, ukuaji wa vipaji, ushirikiano, mshikamano kwa vijana, amani, umoja na afya njema kupitia nguvu ya michezo.





