Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Kuanzisha Mchakato wa Maridhiano-Makamu wa Rais

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Emmanuel Nchinbi amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itaanzisha mchakato wa mazungumzo ya maridhiano ili kuimarisha umoja, amani na mshikamano wa kitaifa. Akizungumza kwa niaba ya Rais, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao Dk. Nchimbi amesema serikali imejizatiti kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuishi kwa utulivu na chini ya misingi ya utawala wa sheria. “Ni dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunaanzisha mazungumzo ya maridhiano ili hata hao wachache wanapata nafasi ya kusikilizwa na kuwa na taifa lenye amani na utulivu,” amesema Dk Nchimbi akiwashukuru viongozi wa SADC.

Dkt Tulia ameonesha ukomavu mkubwa wa kiuongozi - Msama

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Msama Promotion Ndugu Alex Msama amesema ameona Watanzania wengi wakikosoa au kulaumu kitendo cha Dkt. Tulia Ackson kujiondoa kwenye michuano wa kugombea Uspika wa Bunge kwamba labda kuna kitu kibaya, au hatakiwi au amesusa. Msama amesema kujitoa kwa Dkt. Tulia ni jambo zuri linaloashilia ukomavu wake wa kiuongozi na Kidemokrasia, amesema Dkt. Tulia hana kashfa mbaya, sio fisadi, sio mla rushwa bali ameonesha kwa vitendo ubora wake katika Uongozi hadi kuchaguliwa kuwa Rais wa Wabunge wote Duniani. "Amewaachia nafasi wengine waweze kupata baada ya yeye kufanya vizuri katika kipindi chake, inaonesha hana tamaa na madaraka, na kwa uwezo wake mkubwa ni matumaini yangu kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atamteua katika nafasi nyingine kubwa ili andelee kuwatumikia Watanzania' - amesema Msama.

Wabunge Waanza Kujisali

 Waheshimiwa Wabunge Wateule leo tarehe 8 Novemba, 2025 wakijisajili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Kumi na Tatu unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Novemba, 2025.

Vi Agroforesty laandaa maonesho ya kilimo misitu

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Maendeleo la Kiswidishi linalotekeleza miradi ya maendeleo nchini kwa kushirikiana na wabia mbalimbali Vi Agroforesty limeandaa maonesho ya 10 ya kilimomisitu yanayotarajiwa kufanyika mjini Musoma. Meneja Mkazi wa shirika hilo nchini Martha Olotu aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo muhimu linaadhimisha miaka 15 ya mafanikio katika matumizi endelevu ya ardhi, usalama wa chakula na ustahimilivu dhidi  ya mabadiliko ya tabia nchi. Alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 Novemba mwaka huu katika kituo cha mafunzo cha kilimomisitu kilichoko Bweri Musoma na yanatarajiwa kuwaleta pamoja washiriki 6,000. Alisema chini ya kauli mbiu ya ‘kilimomisitu kwa ukuaji jumuishi na endelevu’ maonesho hayo yatakuwa jukwaa la kitaifa la kubadilishana maarifa, mijadala ya kisera, na kuhamasisha ushirikiano wa pamoja . Olotu alisema maonesho hayo yatawakutanisha wakulima, watafiti, watunga sera, wabia wa maendeleo, na sekta binafsi ili kuha...

Mgombea Ubunge wa Ccm Jimbo la Bukoba Mjini Amwaga Shukrani kwa Wananchi

Na Angela Sebastian ;Bukoba  Mgombea Ubunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhandisi Johnston Mutasingwa amewashukuru wananchi wa jimbo hilo, kwa ushirikiano na mapokezi makubwa waliompatia tangu kuanza kwa kampeni za kunadi Ilani ya chama hicho na kuomba ridhaa. Adha amewashauri wajitokeze kwa wingi kesho kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa kupiga kura na kuchagua viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Taifa hadi kata ili waweze kushirikiana kuwaletea maendeleo.  Mutasingwa ameeleza hayo leo wakati akihitimisha kampeni zake katika viwanja vya Shule ya Msingi Kashai ndani ya Manispaa ya Bukoba ambapo amesema kesho ni siku muhimu kwa Taifa letu hivyo, akawaomba wananchi kumuamini na kumtuma kwa kumpigia kura za kutosha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,yeye kwa nafasi ya ubunge na madiwani kwasababu ndiyo chaguo sahii la kutatua kero zao. "Nawaomba mjitokezeni kwa wingi kesho mpige kura kwa amani, utulivu na mchague viongozi wa CCM tutumeni kwas...

Uwekaji Michango Kwa Wakati Kutapunguza Kero ya Mafao Sekta Binafsi

Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. UWASILISHAJI michango kwa wakati utaondoa na kupunguza kero ya malipo kwa waajiriwa wa sekta binafsi pindi wanapoacha kazi au kustaafu. Hayo yamesemwa na meneja wa shirika la mfuko wa hifadhi ya Jamii *(NSSF)* mkoa wa Mara Maneno Mpogole katika hafla fupi ya kuwashukuru wateja kwa ushirikiano wanaoutoa kwa mfuko katika nyanja mbalimbali. Ameainisha nyanja hizo kuwa ni pamoja na kujiandikisha,kulipa michango, kununua au kutumia bidhaa zitolewazo na mfuko ambazo ni nyumba,viwanja,daraja la Mwalimu Nyerere ikiwemo kupanga katika majengo yanayomilikiwa na NSSF yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Mpogole amewahimiza waajiri kuendelea kuwasilisha michango yao kwa wakati kupitia mfumo wa kidigitali ili kuepusha usumbufu kwa wanachama watakaostaafu au kuachishwa kazi kwa kulipwa kwa wakati na kuondoa kero ya malipo kwa wakati. "Kulingana na kasi ya ukuaji wa teknolijia duniani kwa sasa  *NSSF* imeweza kurahisisha huduma zake ambapo waaji...