Uwekaji Michango Kwa Wakati Kutapunguza Kero ya Mafao Sekta Binafsi

GEORGE MARATO TV
0


Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.

UWASILISHAJI michango kwa wakati utaondoa na kupunguza kero ya malipo kwa waajiriwa wa sekta binafsi pindi wanapoacha kazi au kustaafu.

Hayo yamesemwa na meneja wa shirika la mfuko wa hifadhi ya Jamii *(NSSF)* mkoa wa Mara Maneno Mpogole katika hafla fupi ya kuwashukuru wateja kwa ushirikiano wanaoutoa kwa mfuko katika nyanja mbalimbali.

Ameainisha nyanja hizo kuwa ni pamoja na kujiandikisha,kulipa michango, kununua au kutumia bidhaa zitolewazo na mfuko ambazo ni nyumba,viwanja,daraja la Mwalimu Nyerere ikiwemo kupanga katika majengo yanayomilikiwa na NSSF yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Mpogole amewahimiza waajiri kuendelea kuwasilisha michango yao kwa wakati kupitia mfumo wa kidigitali ili kuepusha usumbufu kwa wanachama watakaostaafu au kuachishwa kazi kwa kulipwa kwa wakati na kuondoa kero ya malipo kwa wakati.

"Kulingana na kasi ya ukuaji wa teknolijia duniani kwa sasa  *NSSF* imeweza kurahisisha huduma zake ambapo waajiri, wastaafu,na wachangiaji wa hiari wanaweza  kujichangia,kuhakiki,kufungua madai na kuona malimbikizo ya michango kupitia mfumo kupitia namba ya malipo *( *control number)* pasipo kufika tawi la NSSF na kuokoa muda ikiwemo nauli kwa wanachama", amesema Mpogole.

Hali hiyo imewezesha Mfuko wa NSSF kukua na kuendelea kumudu kulipa mafao ya wanachama wakiwemo wastaafu.

Aidha mfuko umewezesha wanachama kufungua madai ya mafao mahali popote kwa njia ya mtandao(online claim lodging)na kulipwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za mafao pia waajiri wanaweza kujihudumia kwa kuwasilisha na kulipa michango yao kwa kutumia lango la waajiri ( *Employers Portal* ).

Vile vile Wastaafu hawajaachwa nyuma kwa kuwa mfuko umerahisisha na kuwawezesha kuhakiki taarifa zao kwa njia ya mtandao ( *Online Verification)* na hivyo kuwapunguzia adha na nauli kufika katika ofisi za NSSF. 

Maboresho hayo yamekwenda mpaka kwenye marekebisho ya taarifa ambazo haziendani na zilizopo kwenye mfumo wa vitambulisho vya Taifa (NIDA)  na pia kumwezesha mwanachama kuangalia  michango yake kwa kujihudumia mwenyewe kwa kutumia mfumo wa lango la wanachama ( *Member Portal* ).

Mafanikio yote haya yametokana na jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za jamii na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji wa ndani ya mfuko yaliwezesha mfuko kukua na kupandisha kima Cha chini ya Pensheni ya Wastaafu kutoka 100,000 kufikia 150,000 na kuweza kuiishi kauli mbiu ya kimataifa ya mwaka huu inayosema ( *" *MISSION :POSSIBLE"* )

Hakusita kutoa rai kwa waajiri wanaolimbikiza michango na ambao hawajawaandikisha na kuanza kuwachangia wafanyakazi wao kwa mujibu wa sheria  *NSSF* itawafikia  sambamba na kuwachukulia hatua.

Maneno amewakumbusha watumishi wote wa mfuko kuhakikisha wanatumia mfumo huu kujaza utekelezaji wa malengo Yao kwa muda waliopangiwa kwa kuwa serikali ya awamu ya sita imeboresha mifumo ya watumishi kujipima kwa malengo kwa kuandaa mfumo wa *(PEPMIS)* .

Meneja Maneno amewashukuru na kuwapongeza sambamba na kuwatunuku vyeti na zawadi waajiri wanaoweka michango ya wafanyakazi wao kwa wakati na wachangiaji wa hiari wa Hifadhi Skimu wakiwemo wahamasishaji.

Waajiri waliotunukiwa ni *Freegom,Metl Ginning,Al Jaziira Islamic, Diocese of Bishop RC-Mara,Coptic Medical, Shule ya Sekondari Serengeti Nuru,Bunda DDH, Child Ministry,St Paul Bunda, Girls Brigade,St John Bosco,World Changer, Little Flower, Grain to Grow, na Musoma Business.* 

Kwa Upande wa Wachangiaji wa Hifadhi Skimu waliotunukiwa ni Jovina Massano,Juma Issa Julius,Simion Gideon Matiko,Badru Ismail Mashibe na Rehema Majira Rajabu.

Kauli mbiu ya mwaka huu wa 2025 ni " *Kidigitali Tumeweza* "





             

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top