Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Atoa Wiki Moja Kituo Cha Polisi Nandagala Kianze Huduma

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 23, 2025 amekagua ujenzi wa kituo cha Polisi Nandagala, Ruangwa mkoani Lindi na kuagiza kituo hicho kianze kazi ifikapo Novemba 1 mwaka huu. Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Frank Chonya kuhakikisha samani zinawekwa katika kituo hicho ili kiweze kutumika kwa kutoa huduma kwa Wakazi wa Wilaya ya Ruangwa. “Wananchi hawa wanataka kituo hichi kianze kazi, majengo yamekamilika bado viti tu, hatuwezi kurudi kumdai IGP, Mkurugenzi simamia tupate viti hapa, pamoja na kuweka paving katika eneo hili, malengo yetu Novemba 1 mwaka huu kituo kianze kazi” Kwa Upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, John Imori,  amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 164 kilitengwa kwa ajili ya kujenga kituo cha Polisi cha daraja C, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu aliagiza kituo hicho kijengwe kwa mfumo wa force account na fedha nyingine zijenge nyumba za Maafisa wa Polisi. “Tunakup...

Baada ya Kushindwa "Kulitumia" Jwtz Sasa Wamekuja na "Uzushi" Mpya Kwamba Jeshi la Uganda(Updf)Lipo Nchini

George Michael Uledi.  October 23,2025. Wanaharakati wa Chadema  walio Nje ya Nchi (Sweden Kenya na Marekani) wakishirilkiana na Viongozi wa Chadema wa ndani ya Nchi wamekuwa kwenye kutekeleza "mradi" wao ili Nchi iingie kwenye machafuko. No Reforms No Election Part II ndio ipo katika execution kuelelea Uchaguzi Mkuu wa October  29,2025. Malengo Makuu Matatu ya No Reforms No Election ni (I)kuhamasisha maandamano ili(II)kuvuruga Uchaguzi Mkuu October,2025 (III)kuishinikiza Serikali kufanya mabadiliko ya lazima ambayo wanayataka wao(KATIBA MPYA). MPANGO UNACHORWA HIVI👇🏾👇🏾 I.Strategy ya kwanza ilikuwa ni kuchonganisha vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama (JWTZ vs Jeshi la Polisi).Wakasema Jeshi la Wananchi(TPDF)lipo nyuma ya Mwananchi hivyo watu wengi watoke October 29,2025 kwenda kwenye Maandamano na eti hakuna Polisi atakayewagusa. Baada ya kuona Jeshi la Wananchi (JWTZ)limekataa kuwa sehemu ya SIASA kwa matamko mawili ya Kaimu Msemaji Mkuu wa Jeshi,JWTZ wakawa tayari ya...

Waziri wa Mambo ya Nje Ateta na Balozi wa Kenya Nchini

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Isaac Njenga, katika jitihada za kuendelea kuimarisha ushirikiano na kuleta maendeleo kati ya nchi hizo mbili. Wakati wa mazungumzo yao, Waziri Kombo amesisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na Kenya, hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji, miundombinu na nishati, ili kukuza uchumi wa pamoja na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa upande wake Balozi wa Kenya Mhe. Njenga amepongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya mataifa haya mawili jirani na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta za kipaumbele zinazochangia ustawi wa wananchi wa pande zote mbili.

Kampeni ya "Nipitie Tukatiki" inavyohamasisha wananchi kupiga kura Oktoba 29

Na: Dkt. Reubeni Lumbagala Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni moja ya Jumuiya muhimu kwa uhai na maendeleo ya CCM. Misingi mikuu ya Jumuiya hii kutoa elimu na malezi kwa jamii. Elimu ni nyenzo muhimu katika kujenga ustawi na maendeleo ya jamii. Ili jamii ipige hatua za kimaendeleo suala la elimu haliepukiki. Jumuiya ya Wazazi licha ya kuwa ni Jumuiya ya kisiasa lakini inatoa elimu ya masuala mbalimbali katika jamii. Kwa kutambua umuhimu wa elimu katika jamii, Jumuiya hii ina miliki shule zake ili kuchagiza vizuri msingi wake wa kutoa elimu kwa jamii. Sambamba na hilo, Jumuiya hii pia imejengwa katika msingi wa kutoa malezi kwa jamii juu ya masuala mbalimbali muhimu katika jamii. Malezi bora katika jamii yanasaidia kujenga jamii yenye raia wenye maadili mazuri na wanaowajibika, hivyo kusaidia katika kufanikisha maendeleo. Jumatano ya Oktoba 29, 2025, ni siku muhimu kwa nchi yetu ya Tanzania. Ni siku ya Uchaguzi Mkuu. Wananchi wanapata fursa ya kutimiza haki yao ya kikatib...

Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule Zote za Sekondari na Msingi Jimbo la Mtumba Kupatiwa Kompyuta Mpakato

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde, ameendeleza kampeni zake katika Kata ya Ihumwa kwa kueleza mikakati ya kuboresha sekta ya elimu na kuinua uchumi wa wananchi kupitia uwekezaji katika miundombinu ya kijamii na biashara. Katika mikakati yake ya kuboresha elimu, Mavunde amepanga kutoa kompyuta mpakato (laptop) kwa shule zote za msingi na sekondari katika jimbo hilo, kwa ajili ya shughuli za kuchapisha mitihani na matumizi ya walimu wakuu. Mpango huo unatarajiwa kukamilika kufikia mwezi Januari, na unatajwa kuwa ni  wa kipekee katika historia ya elimu nchini. "Kila Mwalimu Mkuu na Mkuu wa shule ofisini kwake atakuwa na kompyuta mpakato kwa shule zote za jimbo la Mtumba, pamoja na Kompyuta na mashine za kudurufu mitihani zile gharama za mtihani mnazotoa wazazi nitazibeba mimi mbunge wenu" amesema Mavunde Kwa upande wa Mtaa wa Chang’ombe, Mavunde amesema kuwa Shule ya Msingi Jenerali Msuguri, ambayo ni miongoni mwa shule kongwe k...

Dkt.Nchimbi Ndani ya Jimbo la Momba,Songwe Akifanya 'finishing'' Mikutano ya Kampeni

PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi alipofanya mkutano wa  katika uwanja wa Tindingoma, kata ya chiteto,Wilaya ya Momba,mkoa wa Songwe  leo Oktoba 20, 2025, katika muendelezo wa mikutano yake ya hadhara ya kampeni za lala salama ya kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025