George Michael Uledi.
October 23,2025.
Wanaharakati wa Chadema walio Nje ya Nchi (Sweden Kenya na Marekani) wakishirilkiana na Viongozi wa Chadema wa ndani ya Nchi wamekuwa kwenye kutekeleza "mradi" wao ili Nchi iingie kwenye machafuko.
No Reforms No Election Part II ndio ipo katika execution kuelelea Uchaguzi Mkuu wa October 29,2025.
Malengo Makuu Matatu ya No Reforms No Election ni (I)kuhamasisha maandamano ili(II)kuvuruga Uchaguzi Mkuu October,2025 (III)kuishinikiza Serikali kufanya mabadiliko ya lazima ambayo wanayataka wao(KATIBA MPYA).
MPANGO UNACHORWA HIVI👇🏾👇🏾
I.Strategy ya kwanza ilikuwa ni kuchonganisha vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama (JWTZ vs Jeshi la Polisi).Wakasema Jeshi la Wananchi(TPDF)lipo nyuma ya Mwananchi hivyo watu wengi watoke October 29,2025 kwenda kwenye Maandamano na eti hakuna Polisi atakayewagusa.
Baada ya kuona Jeshi la Wananchi (JWTZ)limekataa kuwa sehemu ya SIASA kwa matamko mawili ya Kaimu Msemaji Mkuu wa Jeshi,JWTZ wakawa tayari yameharibu mno mipango ya Chadema hasa huu wa maandamano.👆👆lengo hapa lilikuwa ni kupata "Mass Mobilisation " ili watu wengi watoke kwenda kuandamana lakini Jeshi limewakataha.🤣🤣
II.Strategy ya pili sasa ambayo yamekuja nayo juzi na jana mitandaoni ni kutaka kulitumia Jeshi la Wananchi wa Uganda(UPDF) kuwatisha Watanzania wasiende kupiga kura October 29,2025.
Juzi na jana kupitia page ya Mange Kimambi + MARIA Sarungi wanasema eti Wanajeshi wa Uganda 500 wameingia Tanzania kwa ajili ya kuzuia Maandamano🤣🤣🤣
Lengo la mpango huu👆👆ni "kuwatisha" wapiga kura wasitoke siku ya Uchaguzi.
TAFSIRI YAKE NI NINI?👇🏾👇🏾👇🏾
I.JARIBIO la kwanza la kuandamana "limeshafeli" so far😀😀😀🤣🤣🤣
JWTZ imewakana mara mbili ndani ya kipindi kifupi na wameshangaa mpango wao wa "divide & Rule" kati ya Jeshi la Wananchi na Jeshi lq Polisi umekwama.
Wamesoma upepo kuwa uwezekano wa watu kwenda kupiga kura ni mkubwa.UWINGI WA WATU KWENYE MIKUTANO YA SAMIA,UMEWATISHAA.
Ii.JARIBIO LA PILI ambalo wamebaki nalo ndio hilo la kuwatisha watu kwamba ETI Mh Rais,Mama Samia "kakodi" Wanajeshi wa Uganda ili kuja kuzuia maandamano na lengo lao hapa ni kwamba watu waogope ili wasitoke kwenda kupiga kura siku ya October 29,2025.
Mission shift hii👆👆from MOTIVATION YA maandamano mpaka kuja kwenye kuzuia watu wasiende kupiga kura ni PIGO KUBWA KWA MPANGO WAO WA NO REFORMS NO ELECTION.
Ni wazi wanaona kuwa no Reforms No Election kwa sasa haiwezekani kabisa.
MASWALI YA KUJIULIZA DHIDI YA UZUSHI HUU ETI(500) WA JESHI LA UGANDA WAMEINGIZA NCHINI.
I.Kama Wanajeshi wa Uganda 500 wameingia Nchini,je wapo kikosi gani?au wanakaa GESTI GANI??🤣🤣
II.Tanzania ina Wanajeshi Nje ya Nchi kwenye MISSION mbalimbali, je,Mh Rais angetaka kuwatumia asingeweza kuwarudisha "fasta" mpaka aende kukodi Uganda???😅😅😅
III.Yaani Jeshi la Polisi lipo,JWTZ wapo,Jeshi la Magereza lipo,Jeshi la Uhamiaji lipo,zimamoto wapo lakini "kanisa la Mungu(TISS)wapo .
Yaani vyombo vyote hivyo vishindwe kuzuia maandamano mpaka twende Uganda?Uongo mbaya sana jamani.
KWA TAARIFA TU👇🏾👇🏾
JWTZ lipo imara na tayari kwa tishio la aina yoyote lile na wala alijawahi kuwaza na alitowaza kuomba msaada kokote hasa katika jukumu la kudumisha ulinzi wa mipaka na uhuru wa Nchi hii.
Achana na Jeshi la UGANDA KUINGIA NCHINI LKN HATA KUKU 500 WA UGANDA TU HAWAWEZI KUINGIA NDANI YA NCHI HII.
Twendeni tukapige kura October 29,2025 then turudi nyumbani tusubilie matokeo tu.Hawana jipya hawa MAJAMAA.
