Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko Asema Kupiga Kura ni Uwekezaji wa Maisha

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amewaasa wananchi kushiriki katika zoezi la upigaji kura Oktoba 29 ili kuchagua viongozi watakaoweza kutimiza matarajio yao ya kuwaletea maendeleo. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 19, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Lyambamgongo wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. “ Uchaguzi ni uwekezaji wa maisha, kupiga kura na kuchagua viongozi inakupa uhalali wa kudai maendeleo kutoka kwa wale uliowachagua. Mimi huwa nashangaa mtu hapigi kura wala haudhurii vikao vya maendeleo lakini anakuwa wa kwanza kulalamika,” amesema Dkt. Biteko. Amesema wapiga kura wa Kata hiyo 4,600 waliojiandikisha wajitokeze kupiga kura na kuichagua CCM ili katika kipindi cha miaka mitano ijayo iwaletee maendeleo. Ametaja baadhi ya mikakati ya CCM katika Kata hiyo kuwa ni kuwaletea gari ya wagonjwa pamoja na kuf...

Act Wazalendo Waahidi Uwekezaji Kukuza Kipato Kata ya Mwisenge

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Mgombea udiwani kata ya Mwisenge kwa tiieti ya ACT Wazalendo Alphonce Dismas Ochieng  amesema atapambania uwekezaji ili kukuza kipato na kuinua uchumi wa wananchi wa kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara. Ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara akinadi sera zake Septemba 18,2025 uliofanyika katika viwanja vya Mtakuja B ambapo katika sera yake amewaeleza wananchi wa kata hiyo kuwa endapo atapata ridhaa  ya kuwa diwani wa kata hiyo atajitahidi kuhamasisha uwekezaji utakaoongeza ajira kwa Vijana na wanawake wa Kata hiyo. Amesema Kata hiyo ina historia kubwa katika Taifa la Tanzania kwa uwepo wa shule ya msingi aliyosoma hayati baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere lakini huduma za kijamii hazilizishi kwa  hadhi yake. "Miundombinu ya barabara siyo rafiki kiasi ambacho kinakatisha tamaa kwa wawekezaji mfano kipande cha barabara inayoelekea Zahanati ya Mwisenge kuelekea Buhare Kuna mwekezaji kaweka hoteli kubwa na kuwezesha ajir...

Dkt.Nchimbi Atua Rasmi Songea Kusaka Kura za Ccm

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi amewasili Songea, mkoani Ruvuma leo Septemba 19, 2025. Dk Nchimbi ataungana tena na Mgombea urais wa chama hicho, Dkt.Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwasili kesho ambapo watakutana mkoa mmoja tangu Agosti 28, mwaka huu walipozindua kampeni za chama hicho kitaifa mkoani Dar es Salaam.  Baada ya uzinduzi,Dkt. Samia na Dk Nchimbi waligawana maeneo kwenda kunadi Ilani ya CCM na kueleza kile walichokifanya miaka mitano iliyopita na wanachotarajia kukifanya endapo watachaguliwa. Baada ya uzinduzi, Samia yeye alianzia Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora, Kigoma na mikoa mitatu kati ya mitano ya Zanzibar ambayo ni, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja na Kusini Pemba. Dk Nchimbi yeye alianza kwa watani zake kanda ya ziwa mikoa wa Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Kagera, Rukwa, Katavi, Arusha, Kilimanjaro, Tanga na sasa anaingia nyumbani mkoani Ruvuma.

Tarura Wabadilishana Uzoefu na Wahandisi Sekta ya Usafirishaji

  Arusha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea kishiriki katika mafunzo yenye lengo la  kuimarisha usimamizi wa mikataba ya miradi ili kupunguza gharama  na  ucheleweshaji wa miradi. Mafunzo hayo ya siku tano ambayo yamewaleta pamoja wadau muhimu katika Sekta ya Ujenzi wa Miundombinu ya barabara na usafirishaji pamoja na mambo mengine yanalenga  kubadilishana uzoefu katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Mkurugenzi wa Barabara kutoka TARURA, Mhandisi Venant Komba amewasilisha mada ya namna TARURA inavyo tekeleza majukumu yake, mikakati inayotumika katika usimamizi wa miradi, teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa Barabara na changamoto zilizopo katika utekelezaji wa miradi hasa kipengele cha mikataba ikiwa ni sehemu ya kutoa uzoefu wa Wakala huo katika eneo hilo muhimu.  Akizungumza wakati wa uwasilishaji Mhandisi Komba amesema moja kati ya vipaumbele walivyonavyo kama taasisi ni kujengea wataalamu wao...

ACP Mpina atoa mbinu kuzuia uhalifu kwenye miamala ya kifedha

*Na Dawati la Habari Polisi Mwanza* Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Mwanza,Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP) Lwelwe Mpina kwa kushirikiana na Waratibu wa Polisi Jamii wa Wilaya ya Nyamagana na Misungwi mkoani humo amewatembelea wafanyabiashara wa miamala ya kifedha katika Kata ya Mkolani, Nyegezi, Nyashishi na Usagara na kuwaelimisha juu ya mbinu za kuzuia uhalifu kwenye miamala ya kifedha maeneo yao ya kazi. Elimu hiyo imetolewa leo Septemba 19, 2025, ambapo wafanyabiashara wamehamasishwa kushirikiana na Polisi katika kulinda mali zao, kutunza mazingira ya biashara na kuchukua tahadhari dhidi ya matukio ya kihalifu. Akizungumza na wafanyabiashara hao kwa nyakati tofauti, ACP Mpina amewasisitiza kufunga taa za kutosha na kamera za ulinzi (CCTV) kwenye maeneo zilipo biashara zao ili kusaidia ufuatiliaji wa matukio ya uhalifu na utambuzi wa wahalifu.   “CCTV ni silaha ya kisasa. Kwa sasa huwezi kuzungumzia usalama wa biashara bila kuwa na kamera za ulinzi. Zina uwezo wa kusaidia kuf...

Dkt Samia na Dkt Mwinyi Waomba Dua Kwenye Kaburi la Abeid Amani Karume

  Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar Ndugu Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na viongozi wengine wakiomba dua kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar tarehe 19 Septemba, 2025.