Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MwanaFA nitaendelea kushirikiana na wakazi wa Tarafa ya Amani

Na Mwandishi Wetu, Muheza MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA amesema wananchi wa Tarafa ya Amani, hawachagui sura ya mtu bali wanachagua mtu anayejali matatizo yao na ameaahidi kushirikiana nao kwa ajili ya maendeleo. Akizungumza kwenye mkutano wa kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanyika kata ya Zirai kwenye uwanja wa Vijana, MwanaFA alisema watu wa Tarafa hiyo hawachagui mtu mradi wamechagua mwakilishi bali wanachagua mgombea anayejali changamoto zinazowakabili katika tarafa yao na namna anavyozitekeleza. MwanaFA ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alisema katika kura za maoni zilizopigwa  ukizijumlisha zote ni asilimia 96 ya kura alizopata. "Watu wa milimani hamchagui mtu kwasababu nyepesi, mnachagua mtu anayetazama changamoto zenu, lakini pia mtu aliyekuwa karibu na nyie, endeleeni kukiamini Chama Cha Mapinduzi na wagombea wake, naahidi kuendelea kutatua changamoto zenu" alisema Mwa...

Same Yampokea Dkt. Nchimbi

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John  Nchimbi, amewasili Wilaya ya Same kuwahutubia Wananchi wa jimbo la Same Magharibi kwenye mkutano wake mdogo,leo Jumapili Septemba 14,2025 mkoani Kilimanjaro. Dkt.Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anaendelea na Mikutano yake ya kampeni mkoani Kilimanjaro,sambamba na kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Magharibi,Ndugu Dkt.Mathayo David Mathayo pamoja na Madiwani. Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo. Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2...

Wasira Azidi Kuchanja Mbuga, Amwombea Kura Dk. Samia Iringa Mjini, Kalenga

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara,  Stephen Wasira,  amezidi kuchanja mbuga kumnadi na kumwombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo  ilikuwa zamu ya Iringa Mjini na Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa. Akiwahutubia mamia ya wananchi katika mikutano miwili akianzia Kijiji cha Kidamali Jimbo la Kalenga na kuhitimisha Uwanja wa Mwembe Togwa, Iringa mjini, Septemba 13, 2025, Wasira amesema maendeleo makubwa yatashuhudiwa mkoani humo kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030 ndani ya miaka mitano ijayo. Kupitia mikutano hiyo Wasira alimwombea kura Dk. Samia ili aendeleze kasi ya maendeleo aliyoianza miaka minne na nusu iliyopita, pia aliwaombea kura wagombea ubunge Fabian Ngajilo (Iringa mjini) na Jackson Kiswaga (Kalenga) pamoja na madiwani waliosimamishwa na Chama.

Dkt. Nchimbi Atua Mwanga,Awashukuru na Kuomba Kura Kwa Wananchi

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewasili Wilayani Mwanga na kuwahutubia Wananchi wa Mwanga kwenye mkutano wake mdogo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mikutano vya Cleopa Msuya, leo Jumapili Septemba 14,2025 mkoani Kilimanjaro. Mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo, Dkt. Nchimbi amepokewa na wazee na viongozi wa kimila wa Jamii ya Wachaga (Mangi) na kumvalisha mavazi ya Kimila na kusimika kuwa mlezi wa Machifu wa Wilaya ya Mwanga. Baada ya tukio hilo Dkt.Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,aliwahutubia Wananchi hao na baadae aliitumia nafasi hiyo kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwanga Ndugu Ngwaru Jumanne Maghembe Ibrahim pamoja na Madiwani. Dkt.Nchimbi ambaye yuko Kanda ya Kaskazini,anaendelea na miikutano yake ya Kampeni mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Chama Cha ...