Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Dkt Nchimbi Afika Butiama Nyumbani Kwa Baba wa Taifa

 Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi ametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kijijini Mwitongo,Butiama na kuzuru kaburi la mwasisi huyo wa Tanzania na CCM. Dkt.Nchimbi ameingia mkoani Mara hii leo Agosti 30, 2025 akitokea mkoa wa Mwanza ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya watanzania katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.

Nchimbi Amalizana na Mwanza,Aanza Mara Kwa Kishindo

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Mara,akianza kwa kuwasalimia Wananchi wa Bunda mjini leo Jumamosi Agosti 30,2025  mkoani humo kuendelea na kampeni zake  mara baada ya kumaliza mkoa wa Mwanza. Baada ya kuwasalimia Wananchi wa Bunda mjini,Balozi Dkt.Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia aliwanadi Wagombea wa Mkoa huo akiwemo  mgombea Ubunge wa Jimbo la Bunda mjini, Easter Bulaya  pamoja na Wagombea wa Udiwani . Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi yupo kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya Kufanya Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Majaliwa Ataka Mikakati Zaidi Matumizi ya Nishati Safi Kwenye Magereza.*

_Asema Rais Dkt. Samia ameonesha njia kwenye matumizi ya nishati safi._ _Alipongeza Jeshi la Magereza kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo matumizi ya nishati safi._   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati zihakikishe kuwa magereza yote nchini yanaunganishwa na mifumo ya nishati safi ifikapo mwaka 2027. Amesema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itasaidia kuboresha huduma kwa wafungwa, kulinda afya za watumishi na wakazi wa magereza pamoja na kuhifadhi mazingira. ametoa wito huo leo Jumamosi (Agosti 30, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Magereza nchini. Uzinduzi huo umefanyika kwa niaba ya magereza yote nchini. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa uzinduzi huo ni utekelezaji wa mkakati wa kuhama kutoka nishati zisizosafi na kuhamia katika matumizi ya Nishati Safi ya kupikia. “Rais wetu Dkt. Samia anatambulika Afrika na duniani kwa ujumla k...

Dkt Hussein Ali Mwinyi Achukua Fomu Ya Urais Zanzibar

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla ameungana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, viongozi mbali mbali na wanachama wa CCM wakati akichukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar iliyopo Maissara.

Nirc Yakamilisha Uchimbaji wa Visima Mashamba ya Bbt Ndogoye na Chinangali

📍 *Dodoma.*  Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imekamilisha zoezi la uchimbaji wa visima katika shamba la Ndogowe na Chinangali lililoko chini ya Mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT), kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha Umwagiliaji. Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Utafiti na Ukuzaji Teknologia iliyo chini ya Idara ya Usanifu na Utafiti (Assistant Director Research and Technology Promotion)  Mhandisi Naomi Mcharo amesema, Tume imechimba jumla ya visima 72 katika mashamba ya mradi wa BBT yaliyopo mkoani Dodoma.  Amesema kati visima hivyo, 42 vimechimbwa katika Shamba la Chinangali na visima 30 katika Shamba la Ndogowe. Mhandisi Naomi amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha wakulima wanajihusisha na kilimo cha uhakika kinachotegemea teknolojia ya umwagiliaji badala ya mvua pekee. “Kukamilika kwa zoezi hili ni hatua muhimu ya kuimarisha kilimo cha kisasa chenye tija. Hatua inayofuata ni kuendelea na uchimbaji wa visima ...