Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wakulima wabenkika kidijitali mpaka shambani na Azania Bank-Nanenane 2025

Azania Bank imeshiriki katika maonesho ya Nanenane mwaka huu katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Mbeya, Mwanza, Simiyu, Tabora na Zanzibar. Maonesho hayo yalihitimishwa kitaifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma.   Azania Bank imetumia maonesho hayo kutoa elimu ya masuala ya ufugaji msaada na namna benki hiyo inaweza kuwakomboa wakulima, wapitia huduma mbalimbali chini ya kauli mbiu yake ya 'Benkika Kidijitali Mpaka Shambani' ambapo mkulima anaweza kupata huduma za kibenki hata akiwa shambani kwa kutumia simu yake mkononi.

Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt. Samia mazishi ya Hayati Ndugai

*_Asema aliimarisha ushirikiano kati ya Bunge na Serikali_* *_Atoa rai kwa Watanzania kuenzi mema yote aliyoyafanya enzi za uhai wake_* Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 11, 2025 amemwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Job Yustino Ndugai, yaliyofanyika shambani kwake, kijiji cha Msunjulile, wilayani Kongwa mkoani Dodoma. Akizungumza katika ibada ya mazishi, Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuenzi mema yote yaliyofanywa na Hayati Ndugai enzi za uhai wake, akisema mchango wake katika uongozi wa Bunge na Taifa kwa ujumla utabaki kuwa kumbukumbu muhimu kwa vizazi vijavyo. Amesema kuwa akiwa mwakilishi wa wananchi wa Kongwa, hayati Ndugai ametoa mchango mkubwa katika kipindi cha miaka 20 ya utumishi wake, na kwamba wote ni mashuhuda wa maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sekta mbalimbali za maendeleo pamoja na huduma za kijamii. “Serikali itaendelea kumuenzi kwa yale yote aliyoyafanya kwa wanaKongwa” Aidha, Waziri...

Rais Samia kuendesha harambee ya CCM kutafuta Bilioni 100 za uchaguzi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo vya Habari leo Jumatatu Agosti 11, 2025 katika Ofisi Ndogo ya CCM Makao Makuu, Lumumba, jijini Dar es Salaam,kuhusu. harambee ya kuchangia kampeni za chama hicho itakayozinduliwa rasmi kesho katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Harambee hiyo inalenga kukusanya Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya kampeni, ikiwemo gharama za magari, mabango, mafuta, fulana na kanga.

Wasira Ashiriki Kuaga Mwili wa Spika Mstaafu Job Ndugai

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg Stephen Wasira ameungana na waombolezaji kuaga mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Job Ndugai. Wasira ameshiriki kuaga mwili wa marehemu Ndugai katika ibada ya mazishi na uagaji mwili huo kitaifa ulioongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika leo Agosti 10, 2025 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Ibada ya mazishi na uagaji mwili wa Spika Mstaafu Ndugai ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, CCM, taasisi za umma, mashirika binafsi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa. Spika Mstaafu Ndugai alifariki dunia Agosti 6, 2025 jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi na mazishi yake yatafanyika kesho Agosti 11, kijijini kwao Seleji wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma. 

Mwili wa Ndugai wawasili Kongwa Wananchi wafurika kutoa heshima za mwisho

Mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Job Ndugai wawasili Kongwa, Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Wilaya ya Kongwa wajitokeza kwa wingi kuaga mwili wa Spika Mstaafu Job Ndugai katika viwanja vya stendi ya mabasi Kongwa leo tarehe 10 Agosti 2025 Wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Govt, Inter-University Council and stakeholders appreciate NIT’s EASTRIP project implementation

  By Prosper Makene  The government together with the Inter-University Council for East Africa (IUCEA) and World Bank have commended the National Institute of Transport (NIT) on implementing East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP), saying the Institute has progressed well in infrastructure development and capacity building in supporting the aviation and transport sector. . During their visit to NIT main campus in Mabibo, Dar es Salam over the weekend, the Team were pleased with the progress made in the construction of various buildings at the Institute which are now complete at 100 percent. They commended the Institute’s administration team for their exceptional project management skills and dedication in ensuring that the construction meets the set standards. Dr. Cosam Joseph, the Project Coordinator for the EASTRIP at the IUCEA, said: “We are very satisfied with the quality of the work that has been done here, the contractors have don...