Wasira Ashiriki Kuaga Mwili wa Spika Mstaafu Job Ndugai

GEORGE MARATO TV
0

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg Stephen Wasira ameungana na waombolezaji kuaga mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Job Ndugai.

Wasira ameshiriki kuaga mwili wa marehemu Ndugai katika ibada ya mazishi na uagaji mwili huo kitaifa ulioongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika leo Agosti 10, 2025 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Ibada ya mazishi na uagaji mwili wa Spika Mstaafu Ndugai ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, CCM, taasisi za umma, mashirika binafsi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa.

Spika Mstaafu Ndugai alifariki dunia Agosti 6, 2025 jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi na mazishi yake yatafanyika kesho Agosti 11, kijijini kwao Seleji wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma. 





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top