Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Hatua ya Trump kuzima misaada ya USAID itaua watu 14 milioni – Utafiti

 Mataifa 132 Duniani ikiwemo Kenya na Tanzania ambayo yalikuwa yakinufaika moja kwa moja na ufadhili kutoka kwa Shirika la Ustawi wa Kimataifa la Marekani (USAID), ziko hatarini kupoteza jumla ya watu 14 milioni kufikia mwaka 2030 baada ya kufungwa rasmi kwa shirika hilo la kutoa misaada. Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la sayansi la Lancet unaeleza kwa kina jinsi hatua zilizopigwa katika miongo miwili iliyopita kupunguza vifo vya watoto na watu wazima, zitaporomoka. “Makadirio yetu yanaonyesha kuwa, isipokuwa hatua za kupunguza ufadhili zilizotangazwa na kutekelezwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025 ziondolewe, idadi kubwa ya vifo vinavyoweza kuepukika vinaweza kutokea kufikia mwaka 2030,” walisema watafiti. Tofauti na tafiti za awali ambazo zilijikita tu kwenye athari za moja kwa moja za kiafya, utafiti huu mpya umeangazia pia athari mbadala ambazo pia zinaweza kusababisha vifo na kupoteza njia za kujikimu, na kueleza kuwa pia zinaathiri afya ya watu. Mipango isiyo ya ...

Dkt. Biteko Asema Tanzania ina Usalama wa Chakula, Awapongeza Wakulima

📌 Asema Serikali inatambua Vyama vya Ushirika ni muhimu kuunganisha nguvu za wananchi na kujiendeleza kiuchumi 📌 Mauzo ya nje ya kahawa na tumbaku 2023/2024 yaongezeka hadi Dola za Marekani 19,300,000 📌 Maono ya Rais Samia yaanza kuonekana sekta ya kilimo yachangia GDP asilimia 26 📌 Aziagiza Wizara za Fedha na Kilimo kupata ufumbuzi wa bei za mazao Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewapongeza wakulima nchini kwa jitihada zao za kuzalisha mazao kwa wingi na hivyo  kusaidia nchi kuwa na usalama wa chakula  ikiwa ni pamoja na kuwezesha sekta ya kilimo kuwa na mchango mkubwa katika Pato la Taifa.  Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo Julai 5, 2025 jijini Dodoma wakati akifunga Kongamano la Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani. “Leo sekta ya kilimo ina mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi yetu, tunazungumza mchango wa GDP wa asilimia 26, tunazungumza mazao ambayo yanatupa...

Fanyeni Kaguzi Kwenye Maeneo Yaliyohifadhiwa-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameziagiza Mamlaka za Mikoa na Wilaya kufanya kaguzi za mara kwa mara katika maeneo yaliyohifadhiwa, vyanzo vya maji na mito ili kudhibiti vitendo vya uharibifu wa mazingira. Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi Julai 05, 2025) aliposhiriki katika mbio za Great Ruaha Marathon (GRUMA 2025) zilizoanzia na kuishia kwenye eneo la Ibuguziwa, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, mkoani Iringa. “Wekeni utaratibu mzuri wa matumizi ya vyanzo hivyo, tunataka kuona mikondo yote ya maji inayokwenda kulisha mto mkuu, inahifadhiwa ili tupate maji mengi na yaweze kuchangia kwenye shughuli za kimaendeleo, mto Ruaha Mkuu unapeleka maji katika bwawa letu la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere” Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza mamlaka hizo zibainishe vyanzo muhimu vya maji vilivyopo kwenye maeneo yao na kuweka utaratibu maalum na wawazi juu ya namna ya kuhifadhi vyanzo hivyo ili viweze kuzalisha maji ya kutosha. “Mimi ninawasihi wekeni Sheria ndogo zinazodhibiti uharibifu na kutambua ...

Waziri Mkuu Ashiriki Mbio ya Gruma 2025

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Julai 05, 2025 ameshiriki katika mbio za Great Ruaha Marathon (GRUMA 2025) zilizoanzia na kuishia kwenye eneo la Ibuguziwa, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Akizungumza katika tukio hilo, Mheshimiwa Majaliwa ameto wito kwa waratibu wa mbio hizo kuweka mikakati ya kuzifanya ziwe za kimataifa ili ziweze kukutanisha raia wa mataifa mbalimbali duniani. Lengo la Mbio hizo ni kuhamasisha uhifadhi wa mazingira  wa Mto Ruaha Mkuu ambao ni uti wa mgongo wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kuifanya jamii kuona umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na kuhimiza matumizi endelevu ya rasilimali za asili.

Wahamiaji haramu 800 wakamatwa mkoani Kagera

  Na Angela Sebastian  Bukoba Zaidi ya wahamiaji haramu 800 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera ndani ya mwezi Juni mwaka huu ambapo baadhi yao tayari wamerudishwa katika nchi zao na wengine wakifuata taratibu za na sheria za nchi zinavyoelekeza. Mkuu wa Waziri Mkuu wa Habari Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Petro Malima amessema wahamiaji hao wengi wao wanaotumia nchi jirani na huingia kwa njia isiyo rasmi. Amesema kwa kipindi cha mwezi Juni mwaka huu walikamatwa wahamiaji 725,ambao ni raia wa Burundi ni 514,Uganda 59,Rwanda 41,Kenya mmoja DRC sita,Ethiopia mmoja,China watano,Pakistan Watanzania mmoja, 53 na watu wengine ambao walikuwa wanatafuta urahia ni 44. "Unaweza kushangaa kwanini Watanzania, ni wale ambao wanapatikana na makosa kama vile wamekutwa na wahamiaji haramu au makosa ya kawaida ambayo yanaangukia kwenye makosa ya uhamiaji"ameeleza Malima. Amesema wahamiaji wapatao 637 waliondolewa kutokana kutokuwa na shaka nao pia kuhusu waeth...

Rais Ruto:Sitaomba Msamaha kwa Kujenga Kanisa Ikulu

  RAIS wa Kenya Dokta William Ruto amekubali kuwa anajenga Kanisa katika Ikulu ya Harambee Jijini Nairobi akidai kuwa anatumia pesa zake kulijenga. Kiongozi huyo Mkuu wa nchi alisema kuwa yeye anaamini Mungu na kwamba hataomba masamaha kwa kujenga Kanisa la Mungu. Tutajenga kanisa la Mungu, shetani akasirike afanye kile anachotaka,”Rais Ruto alisema. “Ni kweli mimi najenga Kanisa hapa Ikulu kwani nilipata kanisa la mabati.Kanisa la mabati inatoshana na Ikulu? Kwa upande mwingine Dkt Ruto anasema kuwa anatumia pesa zake kujenga hilo kanisa. “Haitagharimu serikali ya Kenya hata shilingi moja kwani najenga na pesa zangu,” akaongeza Dkt Ruto. Haya yanajiri siku moja tu baada ya habari kuhusu ujenzi wa kanisa hilo lenye uwezo wa kusitiri watu 8,000 kufichuliwa kwenye Baadhi ya Vyombo vya Habari Nchini Kenya”. Kulingana na ufichuzi huo, kanisa hilo, lililopambwa kama ‘Cathedral’, linaundwa na Skair Architects Limited na lina madirisha marefu na picha za setilaiti zinaonyesha ujenzi unaoe...