Na Angela Sebastian
Bukoba
Zaidi ya wahamiaji haramu 800 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera ndani ya mwezi Juni mwaka huu ambapo baadhi yao tayari wamerudishwa katika nchi zao na wengine wakifuata taratibu za na sheria za nchi zinavyoelekeza.
Mkuu wa Waziri Mkuu wa Habari Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Petro Malima amessema wahamiaji hao wengi wao wanaotumia nchi jirani na huingia kwa njia isiyo rasmi.
Amesema kwa kipindi cha mwezi Juni mwaka huu walikamatwa wahamiaji 725,ambao ni raia wa Burundi ni 514,Uganda 59,Rwanda 41,Kenya mmoja DRC sita,Ethiopia mmoja,China watano,Pakistan Watanzania mmoja, 53 na watu wengine ambao walikuwa wanatafuta urahia ni 44.
"Unaweza kushangaa kwanini Watanzania, ni wale ambao wanapatikana na makosa kama vile wamekutwa na wahamiaji haramu au makosa ya kawaida ambayo yanaangukia kwenye makosa ya uhamiaji"ameeleza Malima.
Amesema wahamiaji wapatao 637 waliondolewa kutokana kutokuwa na shaka nao pia kuhusu waethiopia,wachina,Pakistan na Drc hao ni wale ambao wanakuwa hawana vibali ila waliingia kihalali na paspoti zao ni nzuri ila muda wao umeisha wanajisahau hao wanapewa utaratibu mwingine.
Amesema warundi 514, waganda 59 na Wanyarwanda 41 hao walikamatwa kutokana na msako ambapo wamerejeshwa kwao kutokana na mahusiano ya nchi za Afrika Mashariki, pia msako huo ni zoezi linalotekelezwa kwa ajili ya kuimalisha usalama wa nchi, maana wakiachwa na kuwapatia mamlaka watakaoshindwa kuchukua hatua yoyote hivyo wanaweza kuibua hoja kuwa walizaliwa Tanzania.
sababu Amesema zinazowafanya wahamiaji kutambua Tanzania kuwa ni pamoja na kutafuta mafanikio makubwa ya miwa na ya watu binafsi kwenye migomba na kahawa.
Ame kuwa kwa mwezi huu wa saba wahamiaji haramu wengine zaidi ya 100 walikamatwa katika operesheni maalum ya kuondoa wahamiaji haramu ili usalama wa mipaka ya Tanzania unalindwa ipasavyo.
Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Malima amewataka wananchi wa Mkoa wa Kagera kuendelea kutoa taarifa kwa vyombo vya habari ili kuwalinda na kuwachukulia hatua watachukua hatua kutokana na watakapo achwa na kubaki katika eneo fulani kwa muda mrefu mwisho watajimiliki ardhi na kujikuta ndio viongozi wa siku za mbeleni.
Mwisho