Samia asema kuanza kwa Tren ya mizigo SGR kutaimarisha Tanzania kuwa lango la biashara Afrika Mashariki
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kwa usafirishaji mizigo katika reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) pamoja na mambo mengine, kutaimarisha nafasi ya Tanzania kama lango la biashara katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Rais Samia ametoa kauli hiyo Juni 27, 2025 alipokuwa anahitimisha shughuli za bunge Jijini Dodoma, akitoa mrejesho wa utekekezaji wa majukumu ya serikali na yale iliyoahidi kufanya hususani kwenye sekta ya uchukuzi.