Na. Edmund Salaho, Kaliua -Tabora Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Nassoro Kuji leo tarehe 21, Juni 2025 amefanya ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Taifa Mto Ugalla iliyopo Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora na kuzindua Jengo la Utawala pamoja na nyumba za watumishi kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya TANAPA. Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa majengo hayo Kamishna Kuji alisisitiza kutunzwa kwa miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu kwa faida ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo. “Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendeleza juhudi za kuboresha miundombinu katika hifadhi hizi mpya kwa kuboresha miundombinu ya barabara majengo ya Utawala hifadhi, Nyumba za Askari pamoja na Vitendea kazi vingine, hivyo, nisisitize kuitunza miundombinu hii ili iweze kutumika kwa muda mrefu”. “TANAPA tuna kila sababu ya kumshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo anaendelea kuiboresha sekta hii ya U...
Marato tv - Sauti ya Jamii