Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa Kuhusu Ualbino

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwaleo Juni 13, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu HAssan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino yanayofanyika katika uwanja wa Mwanga Centre, mkoani Kigoma. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo kimataifa ni ‘Kudai Haki Zetu, Kulinda Ngozi Zetu, Hifadhi Maisha Yetu’.  Aidha, Kitaifa, kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni: “Ushiriki katika Uchaguzi ni Haki Yetu: Kuchagua na Kuchaguliwa, Linda Haki za Watu Wenye Ualbino.”

Waziri Simbachawene Aitaka Takukuru Ikaze Uzi Kwenye Rushwa Ndogo Ndogo

Na. Lusungu Helela - TABORA  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene ameitaka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa kubwa huku akisisitiza mapambano dhidi ya rushwa ndogo ndogo yasiachwe kwani ndizo zimekuwa kero kubwa kwa watu wengi hususan watu wa kipato cha chini katika maeneo ya  huduma za jamii nchini. Amesema ni muda muafaka sasa kwa TAKUKURU kuanza  kushughulikia rushwa hizo ndogondogo  katika maeneo ya masoko, vituo vya polisi, shule, zahanati na maeneo mengine ya umma ambako baadhi ya watu wanajulikana na wamejigeuza bila kutoa chochote huwezi kuhudumiwa. Mhe.Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Mkoani Simiyu wakati akizindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Mkoa ambalo hadi kukamilika kwake limegharimu kiasi cha Sh.milioni 640. Amesema rushwa za namna hiyo zimekuwa zikiwakera watu wengi wa tabaka la chini ambao ndio wengi hali inayochochea wananchi kuanza ...

UWT Tanga yakunwa na uchapakazi wa Mbunge Ummy Mwalimu

Na - Mwandishi Wetu, TANGA Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempongeza Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, kwa uchapakazi na uwajibikaji wake wa kuwaletea wananchi maendeleo na namna anavyoilea Jumuiya hiyo muhimu kwa uhai wa Chama. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilaya ya Tanga, Bi. Moza Seif, katika Baraza lake la Kikanuni lililokaa Juni 12, 2025 katika Ukumbi wa CCM wilaya ya Tanga ambapo pamoja na mambo mengine, Baraza hilo lilikuwa na ajenda ya kusoma Utekelezaji wa Ilani kwa Madiwani wa Viti Maalum wa Jiji la Tanga. Bi. Moza amempongeza Mbunge Ummy Mwalimu ambaye amekuwa bega kwa bega na Jumuiya hiyo katika kusukuma gurudumu la maendeleo ndani ya Jiji la Tanga. Katika kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Mbunge huyo, uongozi wa UWT Tanga ulimpatia Mbunge Ummy Mwalimu Zawadi mbalimbali za Pongezi ambazo zilipokelewa na Bi. Mwanahawa Mwalimu kwa niaba ya Mbunge. Sambamba na hilo, Madiwani wa Viti ...

Wana Ccm Kamnyonge,Nyamatare,Kwangwa Na Nyasho Wamuahidi Kumchagua Mathayo

Na Shomari Binda-Musoma  WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kata za Kamnyonge,Nyamatare,Kwangwa na Nyasho wamemuahidi kumchagua tena mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo uchaguzi ujao 2025. Kauli hizo wamezitoa kwa nyakati tofauti leo juni 12,2025 wakati wa ziara ya mbunge huyo kwenye Kata hizo wakati akipita kuwashukuru kwa kumpa ushirikiano kwa miaka 5. Licha ya kuahidi kumchagua wamemchangia fedha kwaajili ya kuchukua fomu kupitia chama hicho zitakazoanza kutolewa juni 28 mwaka huu. Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kamnyonge Emanuel Bwimbo amemwambia mbunge huyo asiwe na shaka kwa kuwa yale aliyoyafanya wana kila sababu ya kumchagua. Amesema wameridhika na utekelezaji wa ilani uliofanywa na mbunge huyo na hawana sababu ya kutokumchagua uchaguzi ujao. Bwimbo amesema kwenye sekta ya elimu,afya,maji,miundombinu na masuala ya kijamii na Kata ya Kamnyonge wanakwenda kumchagua tena kuanzia ngazi ya chama hadi uchaguzi wa jumla. " Mheshimiwa mbunge tukuahidi tuko pamoja na...

Ni Bajeti yenye matumaini kwa wananchi

Na Saidina Msangi, WF, Dodoma WAZIRI wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewasilisha Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali, ambapo ameliomba Bunge ridhaa ya kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 56.49 kwa Mwaka wa Fedha 2025/26. Dkt. Nchemba ameomba ridhaa hiyo bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26, ambapo bajeti hiyo inatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani ya shilingi trilioni 40.47, misaada shilingi trilioni 1.07 na mikopo ya shilingi trilioni 14.95. ‘‘Kati ya mapato ya ndani yanayotarajiwa, mapato ya kodi ni shilingi trilioni 32.31, mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni 6.48, na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi trilioni 1.68. Aidha, mikopo inajumuisha shilingi trilioni 6.27 kutoka vyanzo vya ndani na shilingi trilioni 8.68 kutoka vyanzo vya nje’’, alifafanua Mhe. Nchemba. Alieleza kuwa makadirio ya matumizi ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka 2025/26 y...

Dkt. Nchimbi Akifuatilia Bajeti Kuu ya Serikali

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akifuatilia Hotuba ya Mapendekezo ya Serikali kuhusu Bajeti Kuu ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 akiwa ofisini kwake, katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, leo Alhamisi, tarehe 12 Juni 2025. Pamoja naye ni maofisa waandamizi wa CCM Makao Makuu.