Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

JICA Yaahidi Kuendelea Kuishika Mkono Serikali ya Tanzania-Majaliwa

_▪️JICA, Benki ya Dunia na AFDB watoa Dola za Marekani mil 516 miradi ya kilimo_ _▪️Washauri elekezi wawili Mjapan na Mtanzaniia wawekwa TIC kurahisha uwekezaji_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) limeihakikishia Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa itaendelea kushirikiana nayo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi. Hatua hiyo imetokana na namna ambavyo Serikali imekuwa ikisimamia kikamilifu matumizi ya fedha mbalimbali zinazotolewa na wadau wa maendeleo likiwemo shirika hilo. Waziri Mkuu amesema “Serikali itaendelea itaendelea kusimamia ipasavyo fedha zote za maendeleo zinazoletwa nchini na kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.” Ameyasema hayo juzi (Jumatano, Mei 28, 2025) alipokutana na Makamu wa Rais wa JICA, Miyazaki Katsura kwenye ukumbi wa Mikutano wa Tachibana uliopo katika hotel ya New Otani, Tokyo nchini Japan akiwa katika ziara yake ya ...

Jela Miaka 30 Kwa Kubaka Mtoto Wake

Mkazi wa Kijiji cha Mwakubilinga, Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, Ndakama Pauline Kisabo (35), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na mahakama ya wilaya ya Kwimba baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 10 (jina linahifadhiwa kwa sababu za kisheria). Hukumu hiyo imesomwa leo Mei 29, 2025 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ndeko Ndeko, katika kesi ya jinai namba 4924/2025, baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka. Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa Serikali,  Juma Kiparo, tukio hilo lilitokea tarehe 9 Februari 2025 katika Kijiji cha Mwakubilinga, wakati bibi wa mtoto huyo alipowamuacha mtoto huyo kwa baba yake ambaye alishatengana na mama wa mtoto huyo ndipo mshatakiwa alimvuta mhanga na kumbaka kisha kumpatia elfu moja ili asilie. Mshtakiwa alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 26 Februari 2025 na kusomewa shtaka la kuzini na maharimu, kinyume na Kifungu cha 158(1)(a) cha Kanuni ya Adhab...

Fanyeni ukaguzi kwa weledi bila ya kumwonea mchimbaji yoyote – Mhandisi Kamando

_Wapendekeza maboresho Kanuni za Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira pamoja na Sheria ya Baruti._ 📍*Mwanza* WAKAGUZI wa Migodi ya Madini  na Baruti wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, kuongeza  ufanisi na kufuata  taratibu na sheria za nchi katika utoaji wa huduma. Hayo yamesemwa leo Fanyeni ukaguzi kwa weledi bila ya kumwonea mchimbaji yoyote – Mhandisi  Kamando na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Hamisi  Kamando jijini Mwanza  wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha wakaguzi migodi na baruti ambacho kililenga kujengeana uwezo ikiwemo kufanya maboresho ya  Kanuni mbalimbali za madini na Sheria ya Baruti. ‘’Tusikubali kuyumba au kuyumbishwa na hatimaye kutolewa kwenye mstari, tuendelee kufuata misingi, weledi na maadili katika utendaji kazi kwa kuepuka rushwa na kushinda vishawishi   na tamaa nyinginezo,’’amesema Mhandisi Kamando na kuongeza, “Nitoe rai, tunatakiwa kuwajibika kwa kuzingatia nidhamu, uami...

Tanroads,Tarura Mara Waahidi Kuvipa Kazi Vikundi Utunzaji Barabara

  Na Shomari Binda-Musoma  WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini( TARURA) na Wakala wa Barabara Nchini( TANROADS) mkoa wa Mara wameahidi kutoa kazi kwa vikundi vitakavyosajiliwa kwaajili ya kutunza na kuhudumia barabara. Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa TARURA mkoa wa Mara Mhandisi William Lameck alipokuwa akifunga mafunzo ya siku 14 kwa wanawake,vijana na makundi maalum watakao hudumia barabara. Amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa mkoa wa Mara katika kuhakikisha wanashirikiana kutunza na kulinda barabara. Meneja huyo wa TARURA mkoa wa Mara amesema serikali inatumia fedha nyingi kwaajili ya ujenzi wa barabara hivyo ni muhimu kuwa na matunzo shirikishi. Amesema serikali katika bajeti zake kwenye ujenzi wa barabara inawekwa asilimia 30 zaidi ya milioni 300 kwaajili ya vikundi vya kijamii vya kuhudumia barabara. Mhandisi William amesema watu 86 waliopata mafunzo hayo wanapaswa kuchangamkia fursa na kuanzisha vikundi kwa haraka ili waweze kupata kazi na kujipatia kip...

Waendesha Bajaj na Bodaboda Dodoma Kunufaika Na Programu ya Gurudumu la Mama

▪️Vijana kupatiwa fursa ya kupata vifaa vya pikipiki na Bajaj kwa unafuu ▪️Vijana zaidi ya 2000 kunufaika na awamu ya kwanza ya Progamu ▪️RC Senyamule awataka kuzingatia sheria ili kupunguza ajali ▪️Mbunge Mavunde awawezesha kufungua SACCOS Dodoma Wasafirishaji abiria kupitia pikipiki na Bajaj Jijini Dodoma wanategemea kunufaika na programu ya 𝙂𝙪𝙧𝙪𝙙𝙪𝙢𝙪 𝙡𝙖 𝙈𝙖𝙢𝙖 inayoratibiwa na kampuni ya RoadMaster kwa lengo la kusaidi upatikanaji wa matairi mapya kwa Bajaj na Bodaboda katika mfumo rahisi ambao utawawezesha kundi hili kubwa la wasafirishaji kupata vitendea kazi kwa urahisi na kwa muda mfupi. Hayo yamesemwa jana Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Programu ya 𝙂𝙪𝙧𝙪𝙙𝙪𝙢𝙪 𝙡𝙖 𝙈𝙖𝙢𝙖 iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule. Akitoa maelezo ya programu,Mkurugenzi wa RoadMaster na Mratibu wa Progamu hii Ndg. Thuwein Makamba amesema lengo kubwa la programu hii ni kuwawezesha wasafirishaji kuwa na matairi yenye ubora ili kusaidia kupunguza ajali zi...

Waziri Mkuu Majaliwa Akutana na Waziri Mkuu wa Japan

_▪️Asema Japan itaendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania_ _▪️Aagiza tathmini ya barabara za Kibiti-Lindi na Morogoro-Dodoma_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Japan, Ishiba  Shigeru ambaye amemuhakikishia kuwa nchi hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania jambo ambalo linalenga kuchochea ukuaji wa uchumi kutokana na fursa zitakazoendelea kupatikana kupitia mahusiano hayo. Amekutana na kiongozi huyo leo (Alhamisi, Mei 29, 2025) katika ofisi ya Waziri Mkuu Tokyo, Japan, ambapo Mheshimiwa Majaliwa amesema ahadi hiyo inazidi kutoa fursa ya wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan pamoja na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kumueleza Waziri Mkuu huyo kuwa  pamoja na miradi mingine wanayotekeleza nchini, Japan kupitia JICA iangalie uwezekano wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuzifanyia ukarabati mkubwa barabara za Mo...