Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Samia Suluhu Hassan Aongoza Kikao Cha Nec

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kilichofanyika katika Ukumbi wa NEC, jijini Dodoma, leo Jumatano, tarehe 28 Mei 2025. 

Makamu wa Rais Ateta Bosi wa Afdb

 Na Ada Ouko, GMTV. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake Dkt. Akinumwi Adesina.  Kando ya Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika katika Hoteli ya Sofitel Ivoire Jijini Abidjan nchini Ivory Coast.

Dkt Nyansaho Aanza Kazi Kwa Kishindo

  Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Dkt. Rhimo Nyansaho, (kulia) amepokelewa Makao Makuu ya PSSSF jijini Dodoma na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru (kushoto), kuanza majukumu yake rasmi kufuatia uteuzi wake uliofanywa Mei 26 mwaka huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Zaidi ya Migodi 13,000 Yakaguliwa

_• Wakaguzi wa Migodi Wajengewa Uwezo_ _• Makusanyo Sekta ya Madini Yavuka Lengo_ *Mwanza* JUMLA ya migodi 13,279 pamoja na bohari za baruti 164 zimekaguliwa nchini kuanzia Julai 2024 hadi Machi 2025. Hayo yameelezwa leo Mei 28, 2025 jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Idara ya Leseni wa Tume ya Madini, Mhandisi Aziza Swedi, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Mhandisi Ramadhan Lwamo, katika kikao kazi cha wakaguzi wa migodi na baruti kutoka mikoa mbalimbali nchini. Amesema kuwa miongoni mwa migodi hiyo iliyokaguliwa ni migodi mikubwa saba, migodi ya kati 46, migodi midogo 13,226 pamoja na bohari za baruti 164. “Kaguzi hizi zimeimarisha Sekta ya Madini na kuongeza makusanyo ya Serikali kupitia maduhuli, hivyo kuchangia katika kuimarisha uchumi na Pato la Taifa,” amesema Mhandisi Aziza. Ameongeza kuwa, “Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ina matarajio makubwa kwa Sekta ya Madini kutokana na mchango wake mkubwa katika Pato la Taifa. Kufikia m...

Ufanisi wa Ukusanyaji Mapato Wailetea Tanzania Maendeleo

Na mwandishi wetu Jovina Massano. UFANISI katika mapato ya kikodi nchini Tanzania kumewezesha uendelezaji wa miundombinu mbalimbali ukiwemo  ushiriki wa sekta binafsi Pamoja na uimarishaji wa masoko ya mitaji na dhamana inayotumika kufadhili miradi hiyo. Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati aliposhiriki majadiliano ya Viongozi wa Juu kuhusiana na Umuhimu wa kutumia Rasilimali za Bara la Afrika kwa ufanisi itakayopelekea  kuchochea Maendeleo.  Majadiliano hayo yaliyofanyika wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika katika Hoteli ya Sofitel Ivoire Jijini Abidjan nchini Ivory Coast. Amesema kutokana na umuhimu wa miundombinu katika mageuzi ya kiuchumi nchini Tanzania, Serikali ilihitaji kufanya kazi zaidi katika kukusanya fedha ya uendelezaji wa miundombinu ikiwemo Reli ya kisasa (SGR) pamoja na barabara kuu ambazo zitaunganisha mataifa mbalimbali...

Waziri Mkuu Aendelea Kuwashawishi Wajapan Kuwekeza Nchini

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameendelea kuwashawishi wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa wa Japan kuja kuwekeza kwenye sekta za kilimo, afya, uchumi wa buluu, nishati, miundombinu, ufugaji na TEHAMA kwani Serikali imeshaboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji. Ameyasema hayo leo (Jumatano, Mei 28, 2025) alipokutana kwa nyakati tofauti na viongozi wa Shirikisho la Wawekezaji katika Sekta za Miundombinu, Shirikisho la Wawekezaji na Wafanyabiashara nchini Japan (KEIDANREN) na Jumuiya ya Wamiliki, Marais na Watendaji Wakuu wa Mashirika na Makampuni wa Japan (KEIZA DOYUKAI).Waziri Mkuu yuko Tokyo nchini Japan kwa ziara ya kikazi.  “Tunakaribisha makampuni ya Japan kuchangamkia fursa nyingi za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania, zikiungwa mkono na mazingira tulivu ya biashara, mageuzi ya sera, na juhudi zinazoendelea za kupunguza urasimu.” Jana, Mei 27, 2025, Mheshimiwa Majaliwa alikutana na Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan (MLIT), K...