WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameendelea kuwashawishi wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa wa Japan kuja kuwekeza kwenye sekta za kilimo, afya, uchumi wa buluu, nishati, miundombinu, ufugaji na TEHAMA kwani Serikali imeshaboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji. Ameyasema hayo leo (Jumatano, Mei 28, 2025) alipokutana kwa nyakati tofauti na viongozi wa Shirikisho la Wawekezaji katika Sekta za Miundombinu, Shirikisho la Wawekezaji na Wafanyabiashara nchini Japan (KEIDANREN) na Jumuiya ya Wamiliki, Marais na Watendaji Wakuu wa Mashirika na Makampuni wa Japan (KEIZA DOYUKAI).Waziri Mkuu yuko Tokyo nchini Japan kwa ziara ya kikazi. “Tunakaribisha makampuni ya Japan kuchangamkia fursa nyingi za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania, zikiungwa mkono na mazingira tulivu ya biashara, mageuzi ya sera, na juhudi zinazoendelea za kupunguza urasimu.” Jana, Mei 27, 2025, Mheshimiwa Majaliwa alikutana na Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan (MLIT), K...