Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wameendelea na kikao leo Mei 24, 2025 jijini Mwanza kikiwa ni kikao cha 210 kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Uhifadhi, Utalii na Uwekezaji, kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali (Mstaafu) George Marwa Waitara. Kikao hicho cha siku 3 kilianza Mei 22, 2025. Kikitanguliwa na vikao vya Kamati tatu ambazo ni kikao cha Kamati ya Utalii na Huduma za Shirika kilichoongozwa na Bw. Athumani Kwariko, Kikao cha Kamati ya Ukaguzi na Utawala kilichoongozwa na CPA (T) Hadija Ramadhani na Kikao cha Kamati ya Uhifadhi kilichoongozwa na Dkt. Robert Fyumagwa kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Maendeleo ya Shirika ambalo limepewa dhamana ya kusimamia jumla ya Hifadhi za Taifa 21 nchini.
Marato tv - Sauti ya Jamii