· *Waaswa kuacha uvivu*
· *Mgodi wa Elianje, injini ya maendeleo Namungo*
WANANCHI wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha uvivu na badala yake wachangamkie fursa zilizopo kwenye sekta ya madini hususani katika mgodi wa kati wa Elianje uliopo kitongoji cha Namungo, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chingumbwa, kilichopo Kata ya Namungo, Abdallah Rashid akielezea fursa zilizopo huko kupitia Sekta ya Madini.
“Fursa zipo nyingi ni uvivu tu wa wananchi wetu, ukiangalia kwenye mgodi huu unaotua wa Elianje Genesis kuna fursa ya kuchunguza masuala, usafi, kupika, kusambaza vifaa vya madini, uchimbaji na uchenjuaji lakini ndio hivyo,” amesema Abdallah.
Aidha, Mwenyekiti huyo amesema uwepo wa mgodi huo umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi kwa kuchimbiwa kisima cha maji ambacho kwa sasa kinahudumia kaya 918, awali na shida ya maji na wananchi walilazimika kutembea muda mrefu kuchota maji.
“Pia, mwekezaji ametujengea shule ambayo kwa sasa ina wanafunzi 79, awali watoto wali umbali mrefu zaidi ya mbio tatu kufuata shule vijiji jirani hali iliyopelekea baadhi ya kuacha shule.
Kwa upande wa Mkuu wa shule ya msingi Chingumbwa iliyopo kata ya Mbekenyela mkoani humo, Joseph Raymond amesema mgodi wa Elianje umejenga ofisi za Walimu, kuwawekea umeme kwa ajili ya darasa la saba na la nne itakayoanza mwaka ujao wa sita wakijiandaa na mitihani ya taifa.
Naye, Meneja wa Mgodi wa Elianje, Philibert Masawe akizungumzia mgodi huo amesema wanajishughulisha na uchenjuaji wa madini ya dhahabu na uchimbaji wa 'green garnet',
Amesisitiza pia Kampuni ya Elianje imejenga kituo cha mfano cha uchenjuaji wa madini ya dhahabu inayotumia teknolojia ya CIP ambayo kina uwezo wa kuchenjua sahani (mwamba) ya dhahabu kiasi cha tani 500 kwa siku.
Amesema pia kiwanda hicho kimeajiri watanzania 300 na kuipongeza Serikali kuweka sera rafiki na sheria ambazo zinavutia kuvutia.






Comments
Post a Comment