OR-TAMISEMI WANANCHI wa Rufiji mikoani Pwani wameeleza kufurahishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati, shule, madaraja na zahanati. WANANCHI hao pia wamempongeza Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa jitihada zake za kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana kwa uhakika na ubora. Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa UWT taifa Mhe. Mary Pius Chatanda aliyoifanya Wilayani Rufiji kwa siku mbili,(Mei 6-7, 2025) kwa lengo la kukagua utetelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020/2025. Mkazi wa ikwiriri Bw. Abdallah Moba amesema jitihada za Mhe. Mchengerwa za kujenga barabara ya Kituo cha Afya Ikwiriri zimewawezesha wananchi kufika kwa urahisi katika kituo hicho ili kupata huduma za afya msingi. Bi. Mariam Hamza ambaye ni Mama Lishe amesema kuwa, kabla ya barabara ya Kituo cha Afya Ikwiriri kujengwa wateja wake walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya vumbi p...
Marato tv - Sauti ya Jamii