Na: Dk. Reubeni Lumbagala Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetimiza miaka minne. Rais Dk. Samia amekuwa na kazi ya kuendelea kazi zilizoanzishwa na mtangulizi wake lakini pia kuja na mikakati yake ili kuendeleza gurudumu la maendeleo ambalo ndiyo wajibu wa serikali kwa wananchi wake. Sekta ya elimu imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kuhakikisha wanafunzi wa Kitanzania wanapata elimu bora itakayowawezesha kuendeleza maisha yao hasa baada ya kuhitimisha masomo yao. Katika kuangazia mafanikio ya elimu nchini, makala hii imejikita kuona uwezeshaji uliofanywa na serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kwa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu ili kuhakikisha wanafunzi hao wanasoma katika mazingira mazuri. KUONGEZEKA KWA FEDHA YA KUJIKIMU Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kuongeza fedha ya kujikimu kwa siku kutoka shilingi 8,500 hadi 10,000. Kutokana na kuongezeka kwa gharam...
Marato tv - Sauti ya Jamii