Kikwete atoa taarifa kwa Waziri Mkuu maandalizi Mei Mosi yamekamilika 100%Rais Samia mgeni rasmi

GEORGE MARATO TV
0

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu -Ridhiwani Kikwete ametoa taarifa kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ya ukamilifu na utayari wa kilele cha Sherehe za Mei Mosi zinazotarajiwa kufanyika kesho Mei Mosi katika Viwanja vya Bombadier, Manispaa ya Singida.


Akizungumza baada ya ukaguzi na kupokea taarifa, Waziri Mkuu ameeleza kuridhishwa na maandalizi na kupongeza maandalizi yaliyofanyika ambapo ameeleza kuwa na viwango vikubwa sana kuliko kupata kutokea.

Wafanyakazi wote wanakaribishwa wananchi wote kuja kusherehekea mafanikio ya miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo pia Rais Samia anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top