_▪️Asema ameimarisha ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa miradi nchini_ _▪️Asema Miaka minne ya uongozi wake ilani imetekelezwa kwa kiwango kikubwa_ _▪️Asisitiza ilikuwa ni miaka minne ya kazi na uwajibikaji_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amempongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio yaliyopatikana katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita ambapo imeshuhudiwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo umetokana na umarishaji wa ukusanyaji wa mapato nchini. “Bila shaka, kila mwananchi ni shahidi wa jambo hili. Hakika Mheshimiwa Rais anastahili pongezi na tunampongeza sana”. “Ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka minne ya kuiongoza nchi yetu kwa mafanikio makubwa. Sote ni mashahidi kuwa, katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake, Ilani ya Uchaguzi imetekelezwa kwa kiwango kikubwa.” Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili ...
Marato tv - Sauti ya Jamii