Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mawakili wa Serikali Wasisitizwa Kuishauri Serikali na Kutenda Haki


📌 Dkt. Biteko asema Serikali inatambua jitihada za  Asasi za Kiraia kutoa  huduma za kisheria kwa Wananchi

📌 Rais Samia apongezwa kwa mageuzi katika huduma za sheria nchini 

📌 Wanasheria wakumbushwa kuwa marafiki wa Mungu  badala ya Mahakama

📌 Dkt. Biteko ataja mikakati ya Serikali kuhakikisha huduma bora za sheria zinawafikia wananchi


Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Mawakili wa Serikali kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma na haki ili kusaidia Watanzania sambamba na kuwa washauri wazuri kwa viongozi wao.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 15, 2025 jijini Dodoma wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali.

“Ombi langu kwenu Mawakili wa Serikali fanyeni kazi yenu kwa kuzingatia taaluma yenu ya sheria na haki, ni wajibu wenu kushauri kwa haki na fanyeni kazi bila kuogopa,” amesema Dkt. Biteko

Amesisitiza “Fanyeni kazi ya kutetea Serikali yenu, nendeni mkaishauri Serikali na wakati wote mkatende haki, ifanyeni haki kuwa rafiki yenu na anayetokea mbele yenu aone haki imetendeka hata watakaopotoka wakihukumiwa waone wanastahili hukumu waliyopewa,” 

Halikadhalika Dkt. Biteko amewapongeza Mawakili hao wa Serikali  pamoja na wadau mbalimbali kwa kuunda na kuendesha Kamati za Ushauri wa Kisheria za Mikoa na Wilaya pamoja na kuendesha Kliniki za Ushauri wa Kisheria bila malipo katika mikoa mitatu ya Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza. 

Vilevile, amesema kuwa Serikali inatambua jitihada zinazofanywa na Asasi za Kiraia, na binafsi katika kuwahudumia wananchi kupata huduma za kisheria. Ametaja asasi na vyama hivyo kuwa  ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society), Legal and Human Rights Centre (LHRC), Tanzania Legal Aid Providers (TANLAP), Legal Service Facility (LSF), Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) pamoja na Watoa Huduma za Msaada wa kisheria kama UNDP na UN Women.

Ametaja  baadhi ya jitihada  za Serikali katika kuboresha sekta ya sheria nchini kuwa kuajiri Maafisa Sheria, Mawakili wa Serikali pamoja na Mahakimu na imekuwa ikiwawezesha watoa huduma za kisheria kwa kuanzisha Huduma za Msaada wa Kisheria, uanzishwaji wa Kamati za Ushauri wa Kisheria, Kliniki za Ushauri wa Kisheria pamoja mafunzo kwa wataalamu wa sheria, ujenzi wa maeneo ya kutolea huduma za kisheria  kwa lengo la  kuhakikisha huduma bora inawafikia wananchi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amemuelekeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kushughulikia changamoto mbalimbali za Chama hicho  cha Mawakili wa Serikali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kupata eneo la kujenga Makao Makuu ya Chama na Vivutio vya Mafunzo kwa Mawakili wa Serikali katika mikoa ya Arusha na Dodoma

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni. Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Rais Mhe. Dkt.  Samia ameimarisha sekta ya sheria kwa kutekeleza masuala mbalimbali mfano   kusaidia uwepo wa haki jinai na  Kampeni ya Msaada wa Sheria ya Mama Samia.

Mhe. Kabudi amesema kuwa umuhimu wa mkutano huo wa Mawakili wa Serikali kuwa ni kutoa fursa kwao ya kukutana na kujadiliana masuala ya kitaaluma, maslahi yao pamoja na kufahamiana.

Amewapongeza waasisi wa Chama hicho kwa kujenga taswira nzuri huku akiwaasa viongozi wengine watakao fuata kuendeleza taswira hiyo na amewataka  mawakili hao kuwa marafiki wa Mungu badala ya Mahakama kwa kutenda haki na kusema kweli wakati wa kutimiza majukumu yao.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hamza Johari amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kukilea chama hicho kwa miaka mitatu na kusema kuwa ni wajibu wao sasa kukilinda na kuhakikisha kinafikia malengo yake.

Pia, amebainisha kuwa kupitia mkutano huo wameidhinisha Mpango Mkakati wa Chama hicho kitakachoufuata na kutekeleza katika kipindi cha miaka mitano.

“Tumetengeneza Mpango Mkakati tunaokwenda kuutekeleza kwa shauku kubwa pamoja na viongozi wapya watakao chaguliwa katika Uchaguzi unaofanyika leo,” amesema Mhe. Johari.

Amesema hadi kufikia Aprili 9, 2025 idadi ya Mawakili wa Serikali waliojisajiliwa katika Daftari la Mawakili wa Serikali imefikia 3,760 kutoka 2,652 waliosajiliwa wakati wa kuanzishwa kwa Chama hicho.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar, Mhe. Dkt. Mwinyi Talib Haji amewaomba  Mawakili na Maafisa Sheria wa Serikali kufanya kazi kwa uadilifu na  kuzingatia sheria ili kujenga jamii imara na kupunguza mizozo katika jamii.

Aidha, amesema taasisi za sheria ziendelee kushirikiana ili kusaidia wananchi na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi za kuhudumia jamii na kuleta ustawi kwa mustakabali kwa maendeleo ya nchi.

Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali, Amedeus Shayo amesema kuwa Chama chao  kimefanikiwa kujenga mfumo wa kielektoniki wa kukusanya ada kwa wanachama pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi zinazoshughilika na masuala ya sheria za ndani na nje ya nchi.

“ Rais Samia ameendelea kuwa kielelezo kizuri cha haki kupitia Kampeni yake ya Msaada wa Kisheria  na Mawakili wanashiriki kutoa huduma za sheria kwa wananchi. Pia, agizo la Rais Samia la Mawakili kuwa walinzi wa uchumi wa nchi kwa kutumia kalamu limeweka msingi wa Chama hiki na umesaidia kuboresha sheria kadhaa mfano Sheria ya Uwekezaji,” amesema Shayo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu na Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia kwa kuzindua Chama hicho mwaka 2022 na kusema “ Chama hiki kama kilivyoanzishwa na malengo yake kitabaki kuwa Chama bora cha kitaaluma kwa sababu Serikali na mawakili walijipanga kuwa nacho na hili ni jeshi la kulinda uchumi wa nchi kwa sheria na kalamu,” 

Mkutano huo uliohudhuriwa na Mawakili wa Serikali kutoka katika Wizara, Wakala na  Taasisi za Serikali,  Mashirika ya umma umeongozwa na  Kauli mbiu “ Utawala wa Sheria katika Utekelezaji wa Majukumu ya Serikaki ni Nguzo Muhimu katika Kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050” 








Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...